Asasi muhimu za usalama nchini NIS na Jeshi la ulinzi la taifa zimeelezea umuhimu wa kuwahusisha wananchi ipasavyo katika masuala ya Usalama wa Taifa.
Kulingana na mujibu wa maelezo ya bwana Haji alisema kuwa kukosekana kwa usalama kwa taifa kwa namna moja au nyingin kunaweza leta hali tete katika jamii na hata kuhatarisha Biashara za watu jambo ambalo si zuri.
Alisema kuwa haki ya wananchi ya kupinga au kususia mambo kutoka kwa utawala ulioko madarakani ni haki ya kila mmoja kutekeleza ila akasisitiza kuwa jambo hilo ni lazima litekelezwe kwa mujibu wa katiba.
'' Kama kitengo cha ujasusi nchini tuna wajibu wa kuhakikisha kuwa tunawafahamisha na kulinda usalama wa nchi kwa manufaa yetu sisi sote, Katika kufanya hivyo tunahakikisha kuwa tunatekeleza haya masuala kwa uwazi na kwa kushirikisha umma ambao ni washikadau muhimu katika idara ya usalama kwa jumla.'' Sehemu ya hotuba ya Noordin ilieleza.
'' Kama ilivyo ada na desturi habari za ujasusi huweza kutekelezwa kwa usiri sana kwa kushughulikia habari ambazo hazifai kuwekwa wazi kwa umma hivyo kujenga na kuimarisha mifumo imara ya usalama wa taifa kwa kuhakikisha kuwa usalama wa wananchi na biashara zao zinatekelezwa kwa mazingira ambayo ni salama''.
Alisema kuwa usalama ni nguzo munhim ya taifa hivyo basi ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo linakisiwa kuweza kuhatarisha maisha ya wananchi bila shaka ni jukumu la Ujasusi kuweza kuingilia kati kwa haraka.
'' Jinsi tujuavyo masuala ya ujasusi kama ilivyo ada hutekelezwa kwa usiri ila yanapotekelezwa kwa usiri haimanishi kuwa ni dhaifu, tunafahamu fika kuwa katika enzi hizi za utandawazi watu hupinga mambo ambayo hawakubaliani nayo ila ni lazima kutokubliana huko kuwe ndani ya misingi ya sheria, watu hutaka habari, majina na maelezo ya kile wanachokitaka'' sehemu ya hotuba ilisimulia.
Aliweza vilevile kusungumzia hali ya usalama katika taifa la Sudan Kusini kwa kusema kuwa kama taifa wako mstari wa mbele kuhakisha kuwa mataifa jirani yanakuwa salama kwa ushirikiano na mataifa yenye nia njema kama Misri, Chad, na Ethiopia hata hivyo aliweza kuzungumzia kuhusu matumizi ya mitandao katika kukabili usalama wa taifa na wa mataifa mengine.
Kwa upande mwingine Komanda wa jeshi la taifa Bwana Charles Kahariri aliweza kuelezea msimamo wao kama jeshi kwa masuala ya taifa na siasa akisema kuwa jeshi huwa halina muegemeo wowote wa siasa na kusema kuwa hata kama Wakenya wanapinga utawala uliopo ni lazima watekeleze kwa kuzingatia katiba.
''Tunapaswa kuafikiana na kuelewana na uongozi uliopo badala ya kushinda tukisema ''Must GO'' ni lazima tufanye hivyo kwa kuangazia sheria sio tu kusema na ilihali nyinyi ndio mliomchagua kila kitu kifanywe kwa kuangazia sheria za taifa''. Kahariri alisema.