logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu maeneo ambayo Kenya Power imeorodhesha kukosa umeme leo, Alhamisi

Umeme utakatizwa katika nyakati tofauti kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

image
na Samuel Maina

Yanayojiri03 April 2025 - 08:06

Muhtasari


  • Kaunti zitakazoathirika ni Nairobi, Meru, Kakamega, Embu, Homa Bay, Kilifi, Uasin Gishu, Turkana, Makueni, Kiambu na Mombasa.
  • Kenya Power inawasihi wakazi walioko katika maeneo yaliyoathirika kuchukua tahadhari zinazostahili.

Kenya Power

Kenya Power imetangaza kukatizwa kwa umeme katika kaunti 11 siku ya Alhamisi, Aprili 3, ili kuruhusu matengenezo ya mifumo yake.

Kaunti zitakazoathirika ni Nairobi, Meru, Kakamega, Embu, Homa Bay, Kilifi, Uasin Gishu, Turkana, Makueni, Kiambu na Mombasa.

Umeme utakatizwa katika nyakati tofauti kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Nairobi

Umeme utakatizwa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika maeneo ya Forest Road, KICD, Jubilee House, Pangani Shopping Centre, KCDF, Northview Road, Chai Road na maeneo jirani. Maeneo mengine yatakayoathirika ni sehemu za Mogotio, Muthithi Road na Wambugu Ojijo Road.

Kiambu

Sehemu za Kiambu zitakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo yaliyoathirika ni 4 Magajo Primary, Farainya, St. Paul Gatuanyaga, Magana Primary, Munyu Girls, Munyu Dispensary, Munyu Police Station, Githima Shopping Centre, Komo Shopping Centre, Juja Farm Athi, Kwa Ruhi, Juja Farm Mukuyu-Ini, Kwa Murage na maeneo jirani.

Mombasa

Baadhi ya maeneo ya Mombasa yatakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Haya ni Danka Petrol Station, Uwanja wa Ndege, Hakika Maize Mill, Transeast, PN Mashru, Blue Jay, Transpare, Kasemeni, Bofu, Mtaa, Roofing Kenya na maeneo ya karibu.

Kilifi

Maeneo ya Kilifi yatakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, yakiwemo Danka Petrol Station, Uwanja wa Ndege, Hakika Maize Mill, Transeast, PN Mashru, Blue Jay, Transpare, Kasemeni, Bofu, Mtaa, Roofing Kenya na maeneo jirani.

Makueni

Kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, umeme utakatizwa katika Maiani Market, Enzai, Mukaa, Bishop Ngala, Nguluni, Watema, Kitandi, Kilome, Nunguni, Mitini, Kavatanzou, Wautu na maeneo jirani.

Uasin Gishu

Wakazi wa Maranatha, St. Jude, Huruma East na maeneo jirani watakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa tisa alasiri.

Turkana

Katika kaunti ya Turkana, umeme utakatizwa kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi alasiri katika maeneo ya Lokichar, Kakong, Kalemngorok, Keekunyuk, Katilu, KWS na Kaputir.

Kakamega

Sehemu za Kakamega zitakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, yakiwemo Malava Market, Kambi Mwanza, West Kenya Sugar, Kimanget Market, Ikoli Market, Kambili Market, Bulovi Market na maeneo ya karibu.

Homa Bay

Umeme utakatizwa katika Homa Bay kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi alasiri. Maeneo yaliyoathirika ni Starige Hotel, Ambros, Shauriyako, sehemu za Sofia East, Sango East, Garage Road, Tourist Hotel, Makongeni, God Bondo, Got Rabour, Nyalkinyi, Olare, Kadel Nyangweso, Homahills, New Bokimai na maeneo ya karibu.

Embu

Umeme utakatizwa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika Mayori, Karimari, Ciambingu, Igumori, Ntharawe, Kirathe, Ciorindagwa, Kabuguri, Karie, Rurie, Newsite, Kiambere na Kariguri Safaricom.

Meru

Katika Meru, umeme utakatizwa kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika Mavis Petroleum Limited Bypass, Kiambogo C/Fact, Mulanthakari, Thimangiri Market, Kithima, Mulanthakari Girls High School, Kagene C/Fact, Thuura C/Fact, Nkoobo C/Fact, Kathithi DEB, Kauthene Market, Kiithe Kauthene, Munithu Primary, Meru Children's Remand Home, Meru Water Treatment Plant, Rwanyange, Ndiine Primary, Ndekero, Thuura, Kambi ya Nyanyua, Giaki, Soko ya Ngombe, Ndurumo, Kathirune, Mbirikine na maeneo jirani.

Kenya Power inawasihi wakazi walioko katika maeneo yaliyoathirika kuchukua tahadhari zinazostahili na kuomba radhi kwa usumbufu wowote utakaosababishwa.


Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved