logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Malala aomba msamaha watu wa Kakamega kwa kuwaambia wamuunge Ruto mkono

Cleophas Malala sasa anawataka wenyeji wa kaunti ya Kakamega kumuia radhi kwa kuwaomba wampigie kura rais WIlliam Ruto.

image
na Japheth Nyongesa

Yanayojiri04 April 2025 - 07:28

Muhtasari


  • Malala kwenye mahojiano na runinga moja hapa nchini ameeleza kwamba anajutia kufanya maamuzi ambayo kwa sasa hajajaleta matunda kwa wenyeji wa kaunti hio.

Cleophas Malala
Aliyekuwa Katibu wa chama cha UDA Cleophas Malala sasa anawataka wenyeji wa kaunti ya Kakamega kumuia radhi  kwa kuwaomba wampigie kura rais WIlliam Ruto.

Malala kwenye mahojiano na runinga moja hapa nchini ameeleza kwamba anajutia kufanya maamuzi ambayo kwa sasa hajajaleta matunda kwa wenyeji wa kaunti hio.

Mwanasiasa huyo ambayo ni seneta wa zamani wa kaunti ya Kakamega amedai kwamba hajaona chochote cha kujivunia kwa wakaazi wa magharibi tangu rais Ruto alipoingia mamlakani.

"Ningependa kuchukua nafasi hii... kuwaomba watu wa jamii yangu msamaha sababu mwaka wa 2022, kidogo niliwaelekaza mahali ambapo sasa hivi ni dhahiri kwamba sio pazuri," alisema Malala.

 "Mimi nilikua na imani nyingi sababu ile sera ambayo rais alituuzia na mimi nikasema kama haya maneno ambayo yako kwenye manfesto yatatimizwa basi jamii yetu itakuwa vizuri." aliongeza.

Wakati huo huo mwanasiasa huyo ametaja ahadi zisizotimia kama changamoto kubwa inayokumba serikali ya Kenya kwanza.

"Alikuja akatuagiza barabara 1000 km, akasema atafufua tena vile viwanda vyetu vya Nzoia na Mumias. Lakini alipofika kule mambo yakabadilika. Kule Magharibi alisema kwamba kwa siku 100 ataweza kuleta mashine mpya katika kampuni ya sukari ya Nzoia lakini sai imeuzwa., alisema Malala.

"Sababu ukipatia mtu kiwanda chako kwa miaka 40 ni sawa na kuuzwa. Kiwanda cha Pan Peper kilipeanwa sai hakifanyi Kazi. Mumias haiko sawa, hizo zilikua ahadi za uwongo."

Malala kwa upande wake ameeleza kwamba watu wa magharibi wametengwa na serikali na hakuna kitu cha muhimu cha kujivunia zaidi ya kukumbushwa kwamba wamepewa kiti cha spika wa bunge la kitaifa.

"Mambo hayafiki kwetu, tunakumbushwa tu, si mmepewa spika, mmepe waziri mwandamizi. Nafasi ya spika hiyo ni kitu binafsi, spika siyo barabara. spika haileti maji. spika ni nafasi ya binafsi ya Moses Masika Wetang'ula," aliweka wazi.

 Ameendelea na kutaja kwamba wanasiasa ambao walielekea ikulu kwa mkutano na rais walishinwa kabisa kujieleza mbele ya rais kuhusu matakwa yao.

"Na mimi nakasirishwa sana na wale wabunge walienda Ikulu, mmekusanyika vizuri lakini ile ajenda ya kupeana kwa rais hakuna. Kitu ambacho tunataka viwanda vya sukari visiuzwe, barabara zijengwe," alieleza mwanasiasa huyo.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved