logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wizara ya afya yatoa elimu kwa vijana kuhusu kujikinga dhidi ya kufanya mapenzi na umri mdogo

Wizara ya afya ilisisitiza kuwa utekelezaaji wa kitaifa wa elimu ya hali za ujana katika masuala ya kufanya mapenzi ni muhimu

image
na Evans Omoto

Yanayojiri04 April 2025 - 12:26

Muhtasari


  • Wizara ilisema kuwa ilikuwea mbioni kuhakikisha kuwa inawalinda vijana dhidi ya kuambukizwa maradhi kutokana na maradhi yanayotokana na kushiriki mapenzi.

Duale

Wizara ya afya ilisisitiza kuwa utekelezaaji wa kitaifa wa  elimu ya hali za  ujana katika masuala ya ngono kwa vijana  ililenga kuimarisha ujana  wao na kuwapa ufahamu mwema.

Wizara ilisema kuwa ilikuwea mbioni kuhakikisha kuwa inawalinda vijana dhidi ya kuambukizwa maradhi kutokana na maradhi yanayotokana na kushiriki mapenzi.

Kanuni hizo zilianzishwa miaka mitatu iliyopita zikilenga kupunguza  vita na mizozo ya wapenzi ikiwemo na kutekeleza mambo ya ubakaji pamoja na kupata mimba za mapema wizara ilidokeza.

Daktari Jacqueline Kisia  mkurugenzi kuhusu masuala  ya uzazi alisema   wizara iliweza kuangazia umuhimu wa kuangazia ukubwa wa historia ya afya na tathimini yake kwa jumla.

Katika kuangazia usambazaji huo asilimia 15 ya watoto walio na umri wa  miaka 10-18 walikuwa wamejifungua . Aliweza kusisitiza kuwa  kama wizara walikuwa wanafanya hima kuhakiksha kuwa namba hio inapungua na akasema kuwa ''watoto hawasitahili kuwa wanapata watoto.'' katika umri wao huo mdogo.

Alikuwa akizungumza na wanahabari kuhusu hamasisho jijini Nairobi chini ya kauli mbiu maalum ya '' step up to access''kampeini.

Daktari Christine Wambugu anayesimamia idara ya ujana na rika alisisitiza kuhusu umuhimu wa uhusiano mwema kati ya wazazi na watoto wao ili kujadili masula ya vijana na kuwaeleza athari za kushiriki mapenzi katika ujana mdogo.

Alisema kuwa wizara ilikuwa wazi kuzindua mikakati faafu na bainifu kuhusu uwazi kuhusu masuala ya mapenzi .

Hata vivyo kibabu maalimu kuhusu masula na mapenzi na ujana kilichapishwa ili kuweza kuwapevusha vijana pammoja na walezi kuhusu masuala ya maopenzi.

 Kuhusu mpangilio huo na utaratibu huo maalumu uliopigiwa upato na mpango wa vijana kutangaza masuala ya upatikanaji wa mimba za mapema miongoni mwa vijana kama jambo ambalo lilikuwa lafaa kushughulikiwa kwa uwazi na kwa umakini sana.

Ni kampeni ambayo ililenga mataifa ya Kenya,Uganda,Malawi,Zimbabwe na Zambia  ambapo kampeni hio ililenga kuhamasisha vijana  kuhusu mimba  za mapema na jinsi ya kujitunza.

Afisa mtendaji kuhusu magonjwa ya vizusi vya Ukimwi  Tandale Songore aliweza kusisitiza umuhimu wa kuelimisha  na kuwapa mwanga wa ufahamu kusuhu mabadiliko yao ya mwili na jinsi ya kujikinga na kuelewa mabadiliko katika miili  zao.

Vilevile afisa huyo aliweza kuelezea  kuwa habari hizi na ujumbe  huo unalegwa  kuhakikisha kuwa unawaafikia wanafunzi katika shule mbalimbali kote nchi.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved