Msemaji wa serikali Bwana Isaac Mwaura alisema kuwa matamshi yake aliyekuwa waziri wa utumishi wa umma Justine Muturi ni kutokana na hasira ya kupoteza ajira.
Alisema hayo alipokuwa akihojiwa na runinga ya NTV Jumatatu asubuhi ambapo alielezea kuwa Bwana Muturi aliendeleza msururu wa mashambuzi ya maneno kuelekezwa kwa rais kwa sababu hayuko ndani ya serikali.
Bwana mwaura alisema kuwa iwapo una mambo ambayo hayakufurahishi katika serikali unalistahili kuelezea malalamishi yako ndani ya vikao vya baraza la mawaziri ambalo huongozwa na rais .
Kwa kufanya hivyo ungekuwa unatiii na kuheshimu hatikiapo ya kulinda na kuheshimmu katiba ya taifa, bali sio kuishutumu serikali na ilihali upo ndani yake.
''Ikiwa wewe ni kiongozi na unaifanyia serikali kazi hupingi serikali hiyo moja kwa moja la hasha kuna vikao vya baraza la mawaziri ambapo masuala ya ndani huweza kuzungumziwa na kama kuna shida au tofauti hapo ndio mahali pema pa kujielezea si nje'' bwana Mwaura alisema.
'' ikiwa kwa namna moja au nyigine ujikute au ipatikane kuwa hupendezwi na sera za baadhi ya viongozi au jambo linalozungumziwa hukubaliani nalo hustahiki kutoka nje na kuanza kuzungumzia tukio bali njia sawa ni kuhakikisha kuwa unajiuzulu kutoka mamlakani, na watu wengi wamefanya hivyo siku za awali.
Kuhusu suala la maendeleo katika sehemu zote za taifa ambapo wanahabari walitaka kujua ni jinsi gani maendeleo huweza kusambazwa kote nchini.
Mwaura alisema kuwa kuhusu suala la maendeleo, raisi huweza kuwa na timu yake ya ukaguzi wakiwemo makatibu wake ambao huzunguka na kuweka miradi maalum kipaumbele ili kuhakikisha kuwa miradi ambayo ina umuhimu inshugulikiwa mbele kabla.
Vilevile aliweza kuulizwa kuhusiana na matamshi ya Bwana Muturi kuwa mawaziri huwa wanatishwa na usimamizi kauli ambayo alikanusha kwa kusema kuwa Ruto ni kiongozi mwenye maamuzi mapevu na huhakikisha kuwa kila mtu anapewa nafasi ya kujieleza bila kushututishwa.
Vilevile aliweza kusema kuwa kutokana na mikakati na mienendo ya rais ya madili kuwa rais hana uwezo wa kuongoza taifa kutokana na makosa ya kukisiwa kuwa yeye mi mfisadi alikanusha kwa kusema huo ni uongo rais ana historia pana ya uongozi bora tena wa kuaminika vyema bwana Mwaura alisema.