
Aliyekuwa Naibu wa rais Rigathi Gachagua anaonekana kusisitiza kuwa angali imara licha ya kutendewa madhila mengi.
Bwana Rigathi aliendeleza msururu wa kuikosoa serikali huku akionyesha msimamo wake kwa watu wa Kenya pamoja na kwa watu wa Mlima Kenya Kuwashiria kuwa hawatishiki wala kubabaika na ziara ya rais Eneo hilo.
Akichapisha katika mtandao wake wa X, Gachagua aliweza kuandika kwa kusema," .''Kama taifa tunahitaji makuu sio masuala ya kuchochewa na serikali ya vita, sio uchumi ulioangamizwa wala sio ufisadi, sio idara za eilimu ambazo hazifanyi kazi, sio tasisi za afya ambazo hazifanyi kazi wala sio kuwanyima watu uhuru ambao upo katika katiba na mauaji ya kinyama ya vijana wetu na vile uhusiano mbaya wa kidiplomasia na vilevile sera mbovu za kimataifa za nje'' Gachagua aliandika katika mtandao wake.
Aliweza kusema kuwa Kama taifa hatuwezi salia katika giza la kuweza kuongozwa kwa kutumia uongozi wa kiimla na wenye nguvu kwa kulazimishiwa mambo hapa na pale.
''Taifa letu haliwezi likaongozwa na na watu wachache au kundi fulani kwa malengo yao ya binafsi na vilevile taifa liliojaa misingi mibovu ya sheria kwa kukosa utaratibu unaofaa kwa kufuata sheria'' Gachagua alisema.
Gachagua alisema hayo siku moja tu baada ya kuvamiwa na makundi ya vijana waliokuwa wamejihami waliomvamia alipokuwa akihudhuria ibaada katika kanisa la PCEA Mwiki Kasarani siku ya jumapili ya tarehe 6 Aprili, 2025.
Hata hivyo hiyo inajiri siku moja baada ya Rais Ruto kukamilisha ziara yake ya siku tano eneo pana la Mlima Kenya na hivyo basi kujihakikishia uuungwaji mkono kutoka kwa wakaazi wa Mlima baada ya kuzindua na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Bwana Rigathi Gachagua mwanzoni mwa mwaka huu alikuwa ametoa taarifa kuwa kabla ifike mwezi wa tano atakuwa ametoa msimamo wa kuzindua chama na vilevile kuwahakikishia kuwa anawapa mwelekeo na msimamo wa wakazi wa eneo lake la Mlima Kenya Jinsi alivyoahidi
Usiku wa leo Gachagua atakuwa katika Runinga ya KTN ambapo anatarajiwa kutoa taarifa ya msimamo wake kwa taifa na jinsi alivyojipanga kisiasa.