

Seneta wa Kisii Richard Onyonka amesema kuwa serikali za kaunti hazifanyi vyema kama ilivyotarajiwa.
Kulingana na usemi wake Onyonka alisema kuwa kulingana na matumaini mengi yaliokuwa katika wakaazi pamoja na wananchi wengi walikuwa na matarajio mengi kuwa Serikali za kaunti zingerahihishia wananchi huduma.
Onyonka alisema kuwa baada ya serikali hizo kugatuliwa na kupewa majukumu mbalimbali ya kutekeleza halikadhalika kuwa na bajeti yake rasmi bado kuna matatizo mengi yanayozikumba.
''Serikali zetu za Kaunti bado zina safari ngumu ya kutekeleza pamoja kuhakikisha kuwa zinajikwamua kutoka kwa mitego ya madeni na utumizi mbaya wa pesa za umma ili kuhakikisha kuwa miradi na maendeleo inapatikana kwa wananchi bila mizozo wala mikwamo ya mara kwa mara.
Katika viwango tulivyofikia kwa sasa Kaunti hazifanyi vizuri na tulikuwa tunatarajia kuwa kufikia sasa maendeleo katika ngazi ya Kaunti yangekuwa yameshamiri na kuleta mwamko mpya kwa raia jinsi ambavyo watu walikuwa na matumaini makubwa ya katiba yetu pamoja na serikali za Kaunti.'' Onyoka alisema.
Katika serikali za kaunti kuna masuala mengi ambayo yaligatuliwa kama afya, ujenzi wa barabara, maji na masoko mambo ambayo yalikuwa yakitekelezwa na serikali kuu.
Hata hivyo baada ya hayo yote bado kuna matatizo mengi ambayo yanasumbua usimamizi na udhibiti imara wa serikali hizo.Mgao wa bajeti kutoka kwa serikali kuu uliweza kucheleweshwa kwa mwezi wa Pili na tatu wa mwaka wa 2025-2026.
Mwenyekiti wa kamati ya bajeti wa baraza la magavana nchini bwana Fernandes Barasa aliweza kusema kuwa Baraza hilo lilikuwa na nakisi ya upungufu wa ahilingi bilioni 63 pesa ambazo kaunti zilikuwa zinadaiwa ili kuhakikisha kuwa zinatekeleza mipango yake na kuendeleza usimamizi wake vyema.
Wakati huo huo mambo hayo yanaposhughulikiwa ya utepetevu wa serikali za kauntti kuna mzozo wa uongozi ambao ulichipuka katika kaunti ya Nyamira ambapo mabunge mawili ya wawakilishi wadi yaliweza kutengenezwa na kuweza kutangaza misimamo yake kuwa kila bunge lilikuwa halali kisheria.
Mabunge hayo yamekuwwa yakisisitiza kupata mgao wa bajeti kutoka kwa afisi ya mdhibiti wa bajeti ya serikali ili kila moja iweze kuendeshashughuli zake za serikali.
Mizozo miongoni mwa Magavana pamoja na wawakilishi wadi imekuwa ikishamiri na kusababisha baadhi ya Magavana Kutimuliwa ofisini.
Kwa sasa kinachosubiriwa kuhusu hatima ya Kaunti ya Nyamira ni kuona ikiwa bunge la Seneti litaweza kuangazia hoja ya kuweza kujadili kuvunjiliwa mbali kwa gatuzi hilo kupitia kwa maamuzi ya rais.