
KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Aprili 10, 2025.
Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Murang'a, Nairobi, Kiambu, Kirinyaga, Kisii, Siaya, na Kakamega.
Katika kaunti ya Murang'a, maeneo ya Githingiri, Kandara Industrial Park , Rwathe, Gacharage, Muruka, Naaro, Ngararia, Kirwara, na Gatunyu yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Mwiki, na Karen katika kaunti ya Nairobi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Ndekei, Old Kiambu, na Ndumberi katika kaunti ya Kiambu zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Kirinyaga, maeneo ya Kiamaina, Gathuthuma, na Kagumo Sec School yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Eberege Tea Factory, Kenyoro, na Nyabitunwa katika kaunti ya Kisii zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Soko ya Uranga katika kaunti ya Siaya itakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Soko ya Harambee katika kaunti ya Kakamega pia itaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.