logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Saba wafariki katika ajali ya barabarani Kiambu

Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa mbili asubuhi, takriban kilomita moja kutoka eneo la ajali nyingine mbaya iliyotokea Alhamisi jioni.

image
na Davis Ojiambo

Yanayojiri11 April 2025 - 11:58

Muhtasari


  • Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa mbili asubuhi, takriban kilomita moja kutoka eneo la ajali nyingine mbaya iliyotokea Alhamisi jioni.
  • Gari lilitumbukia kwenye mteremko mkali na kubingiria mara kadhaa.
  • Abiria watano walifariki papo hapo, huku wengine wawili wakifariki dunia wakati wakipokea matibabu. 

caption

Watu saba walipoteza maisha yao mapema siku ya Ijumaa baada ya matatu ya abiria 14 kupoteza mwelekeo katika eneo la Kamandura kwenye barabara kuu ya Nairobi-Nakuru.

Gari lilitumbukia kwenye mteremko mkali na kubingiria mara kadhaa.

OCPD wa Limuru Mary Gachie alithibitisha kisa hicho na kusema kuwa matatu hiyo ambayo inamilikiwa na Kijabeline Sacco ilikuwa ikisafiri kutoka Nairobi kuelekea Kijabe.

Abiria watano walifariki papo hapo, huku wengine wawili wakifariki dunia wakati wakipokea matibabu. Watu wanne walionusurika, wote wakiwa katika hali mbaya, kwa sasa wanapokea matibabu katika Hospitali ya Tigoni.

Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa mbili asubuhi, takriban kilomita moja kutoka eneo la ajali nyingine mbaya iliyotokea Alhamisi jioni.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved