Ni mchezo uliotarajiwa kuigizwa katika mashindno ya kitaifa katika kaunti ya Nakuru mnamo Aprili 10, 2025.
''Shule ya kitaifa ya wasichana ya Butere inapatikana katika gatuzi la Kakamega na inajulikana kwa ujuzi wa kipekee kwa kuunda drama za kipekee na za kuvutia kote nchini hasa katika michezo ya kuigizwa.
Mchezo wa kuigizwa mwaka huu katika mashindano ya Drama uliopewa jina Echoes of War uliweza kuleta hali ya sin tofahamu na mwingiliano wa vita kati ya serikali na shule hiyo kutokana na maudhui ya mchezo huo na asasi za sera za usalama wa taifa.
Wakati ambapo mchezo huo ulipoigizwa katika kiwango cha eneobunge waamuzi wa mashindano hayo waliamueleza mwandishi wa mswaada huo kuondoa baadhi ya vifungu ambavyo vinaleta mkinzano wa kimasilahi barua ilifafanua.
Katika kiwango cha Kaunti mchezo huo wa kuigizwa haukukuwa na athari zozote wala usemi mbaya na uliamuliwa uweze kusonga katika kiwango cha mkoa, katika kiwango cha mkoa mswada wa mchezo huo ,uliweza kuongezwa maneno mengine ya uhasama ndani yake.
Kwa kuweza kubaini hilo kuwa mswada uliweza kuongezwa maneno mengine usimamizi wa shule uliafikia uamuzi kuwa mchezo huo usichezwe katika kiwango cha kitaifa kwa kuwa ungeleta masuala ya ukinzani na sera za serikali.
Sheria ya udhibiti namb ri 19.2 ya sheria za drama inasema kuwa mageuzi yoyote katika mswada wa uigizaji ni lazima uwe mdogo sana na iwapo utafanya mabadiliko bila wakaguzi na waamuzi kujua bila shaka mswada huo utaweza kufutiliwa mbali.
Shule kubaini kuwa mswada huo ulikuwa umebadilishwa kwa namna moja au nyingine shule haikupeleka ukaguzi wa mswada huo kwa katibu mkuu wa usimamizi wa ngazi ya maeneo kwa ukaguzi na ukubalisho.
Kama ilivyo ada ya sheria ni kuwa iwapo mswada wa uigizwaji unakosa kufanyiwa ukaguzi katika hicho kiwango cha mkoa bila shaka unatemwa nje kulingana na sheria.
Hata hivyo Mahakama moja Kisii na nyingine maeneo ya Kakamega zilikuwa zimetoa amri ya kuwaruhusu wanafunzi hoa kuendelea na uigizaji wa tamthilia yao ya ECHOES OF WAR.
Ila kulingana na sheria za Muziki na Drama hairuhusiwi mtu wa nje kando na mamlaka ya shule kuweza kuendeleza ukufunzi wowote kwa kisingizio kuwa ni mwelekezi wa michezo ya kuigiza.
Kwa hivyo kujihusisha kwa Cleophas Malala katika mchezo huo wa kuigizwa ilikuwa ni kinyume cha sheria za Drama na muziki kulingana na kifungu nambari 9 (c)cha sheria za Drama'' wizara ya elimu ilitoa maelezo hayo kupitia kwa barua rasmi.