Rais wa Burkina Faso Ibrahim Traore alijibu tetesi na Vitisho kutoka Marekani vya kumtaka asidhulumu raia kwa manufaa yake binafsi .
Traore katika taarifa yake alieleza akisema kuwa wao kama taifa la Burkina Faso wana jukumu na wajibu wa kuhakikisha kuwa wanalinda maslahi ya taifa lao ipasavyo.
Traore kulingana na mujibu wa maelezo yake aliwashujahisha wananchi kwa kuwaelezea kuwa afua zilikuwa ni mbili za kujinasua kutoka kwenye hali ambayo walikuwa ndani yake.
Aliweza kusema kuwa kulingana na mambo yalivyokuwa wananchi walikuwa na chaguo mbili kuamua mustakabali wa maisha yao ya mbeleni.
Aliweza kusema kuwa wananchi walikuwa na jukumu la kupigania haki na uhuru wa taifa lao au wasalie watumwa milele alisema kuwa kuna watu ambao ni watumwa wa akili ili kuweza kuwahudumia wakuu wao.
Alisema kuwa kuna watu ambao wanahitalifiana na uhuru na uzalendo wa taifa la Burkina Faso ambapo huchukua ari ya moyo na uzalendo kuweza kupigania taifa lao.
''Kuna baadhi ya watu ambao wanatupiga vita na kuhakikisha kuwa taifa letu linasambaratika lakini tunawahakikishia kuwa tutapigania haki zetu hadi tamati.
Kuna haya mashirika ambayo huitwa NGO ambayo huendeleza injili ya kusema kuwa yanasaidia watu hayo mashirika ndio yaliyoangamiza taifa la Libya.
Gaddafi yuko wapi walimwangamiza kwa sababu waliona alikuwa amepevuka akili na kuwa kiongozi ambaye alikuwa na maono mapevu kuweza kuhakikisha kuwa wananchi wa taifa lake wanaishi vizuri, haohao wazuri walimwangamiza.
Kwa hivyo kumekuwepo na vita duniani hasahasa vita vya pili vya dunia ambapo mataifa mengi duniani yaliweza kupigania uhuru wake na kuwa katika uongozi uliohuru.
Taifa hili ambalo lilipiganiwa na mababu ambao hawakukuwa wazawa wa taifa hilo kwa sasa baada ya kupevuka wanaanza kutoa muongozo kwa mataifa mengine kwa kutoa vitisho.
Kama taifa tusimame imara na tuhakikishe kuwa tunalinda taifa letu dhidi ya maadui ambao wanania ya kuja kutupora raslimali zetu na kutuacha tukiwa masikini wa kutupwa.
Ni lazima tusimame imara na tuhakikishe kuwa hatutingiziki kwa vyovyote vile hio ndio itakuwa nguzo na malengo ya taifa letu'' Traore alisema.