Cornelius Oduor Naibu mkurugenzi mkuu katika shirika la kutetea haki za binadamu la KHRC alisema kuwa serikali ina rekodi mbovu ya utendakazi .
Cornelius alikuwa akihojiwa na runinga ya Citizen kuhusu hali ya utendakazi wa serikali pamoja na ushirikiano na makundi pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu.
Kulingana na mujibu wa maelezo yake Oduor aliweza kudunisha utendakazi wa serikali katika kushughulikia maswala ya haki za binadamu kwa kuipa serikali kiwango cha chini cha rekodi ya utendakazi.
Alifafanua akisema kuwa lilikuwa ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa lalama na kesi zote ambazo zishawahi ripotiwa kuhusu mauaji ya kutatanisha na ambazo zilihusisha raia na maafisa wa usalama ziwe zimeshughulikiwa kufikia sasa.
Kulingana na maelezo ya Oduor alisema kuwa haki ilikosekana kwa wananchi wengi kutokanna na serikali kutokuwa na azma ya kuwahakikishia haki wale wote waliopoteza wapendwa wao.
Alisema kuwa matukio ya maandanamo yaliyofanyika mwaka wa 2024 Juni 26 yaliyosababisha vijana wengi wa kizazi cha Gen Z kuweza kupoteza maisha yalikuwwa ni matukio ya kusikitisha na ambayo kwa mtazamo wake kufikia sasa haki ingekuwa imepatikana pamoja na wahusika kuwajibishwa ipasavyo.
''Ukiniuliza mbona polisi kufikia sasa hawajawaajibisha na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika kinyume cha kisheria kwa kuwaangamiza vijana takribani 67 waliouawa wengine kwa mtutu wa bunduki.
Kufikia leo inasikitisha kuwa hamna jambo wala kesi yoyote au hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya wahuska hao hiyo ni kuumanisha kuwa polisi hawafanyi kazi kulingana na mujibu wa sheria na jinsi tunavyojua wanastahilikuwa wametekeleza wajibu wao ipasavyo.
Kufikia sasa ni mwaka mmoja hamna lolote lililojiri licha ya rais kutoa ahadi kuwa polisi watatengewa bajeti yao na kutekeleza mambo yao bila kuingiliwa na mtu yeyote lakini tunachokishuhudia kwa sasa ni kinyume cha hali ya juu sana.
Swala la asasi huru kutekwa nyara na serikali ili zitekeleze kazi yake kulingana na mapenzi ya serikali huo ni mkondo hatari kwa taifa kile ambacho kinastahili kuwa kinatekelezwa kufikia sasa ni kuwa familia za wale wote ambao walipoteza wapenzi wao zinalilia haki kwa hivyo ningeomba serikali iwajibike ili tuweze kujua wote waliotenda kinyume na sheria waweze kukabiliwa na mkondo wa sheria'' Bwana Oduor alieleza.