logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bilionea mbilikimo Grand P ajinyakulia kipenzi kipya baada ya kumtema Eudoxie Yao (+picha)

Grand P amejitosa kwenye mahusiano na mrembo mwenye asili ya Asia.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri07 April 2023 - 05:46

Muhtasari


•Mahusiano ya Grand P na Yao yalifika kikomo mapema mwaka jana kwa njia isiyoeleweka baada ya wawili hao kuchumbiana kwa takriban miaka mitatu.

•Wawili hao wamekuwa wakisafiri katika nchi tofauti pamoja na kujivinjari pamoja katika sehemu mbalimbali nzuri.

Mwimbaji tajiri kutoka Guinea, Moussa Sandiana Kaba almaarufu Grand P anaonekana kusonga mbele na maisha yake miezi kadhaa baada ya kutengana na mwanasoshalaiti maarufu wa Ivory Coast, Eudoxie Yao.

Mahusiano ya Grand P na kipusa huyo mwenye umbo la kustaajabisha  kweli yalifika kikomo mapema mwaka jana kwa njia isiyoeleweka baada ya wawili hao kuchumbiana kwa takriban miaka mitatu.

Katika siku za hivi majuzi,mwanamuziki huyo bilionea kutoka Guinea amekuwa akionekana na mwanadada mwingine mwenye asili ya Kiasia, Yubai Zhang, ambaye anaonekana wazi  kuwa mpenzi wake mpya.

Wawili hao wamekuwa wakisafiri katika nchi tofauti pamoja na kujivinjari pamoja katika sehemu mbalimbali nzuri.

"Niko pamoja na mpenzi wangu Grand P, safari yangu nyingine inakuja hivi karibuni," Bi Zhang alisema siku kadhaa zilizopita kwenye video iliyomuonyesha akifurahia muda na mwimbaji huyo mbilikimo.

Siku ya Alhamisi, Grand P alithibitisha mapenzi yake na mrembo huyo wa Kiasia na kuweka wazi kuwa hakuna nafasi ya watu wenye wivu maishani mwao.

"Yubai Zhang wangu, hakuna nafasi kwa watu wenye wivu," alisema chini ya picha zake na Zhang alizochapisha Facebook.

Haya yanajiri  miezi kadhaa tu baada ya bilionea huyo kujigamba kuhusu uhusiano wake usioweza kuvunjika na Eudoxie.

Mapema mwaka jana, Grand P aliweka wazi kuwa ataishi kumpenda mrembo huyo aliyebarikiwa na makalio makubwa kweli katika siku zote za maisha yake.

"Wewe na mimi ni kwa maisha. Shukran" Grand P alimwandikia Bi Yao.

Mwanamuziki huyo alisisitiza kuwa ndoa yake na mwanasoshalaiti huyo kutoka Ivory Coast ni imara na ya kudumu.

"Wanandoa wa milele, upendo wetu ni dira ya wenye wivu" Grand P alisema.

Mwanamuziki huyo mwenye maumbile ya kipekee aliendelea kumsherehekea mpenzi huyo wake wa zamani kwa jumbe tamu za mapenzi hadi mahusiano yao yalipogonga ukuta wakati usiothibitishwa mwaka jana.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved