logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Manzi wa Kibera adokeza anatarajia mtoto na mpenzi wake wa miaka 67

Manzi wa Kibera alionekana kusherehekea penzi lake na anayedaiwa kuwa mpenzi wake mwenye umri wa miaka 67.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri25 October 2023 - 07:11

Muhtasari


•Manzi wa Kibera alionekana kusherehekea penzi lake na anayedaiwa kuwa mpenzi wake mwenye umri wa miaka 67.

Mwanasosholaiti maarufu wa Kenya Sheriffa Wambui almaarufu Manzi wa Kibera amedokeza kwamba ana ujauzito wa mtoto wake wa kwanza.

Siku ya Jumatano,  mwanasholaiti huyo kutoka Kibera alichapisha picha yake na mzee anayedaiwa kuwa mpenzi wake akiwa ameshika tumbo lake lililochomoza.

Ingawa hakushiriki maelezo mengi kuhusu ‘ujauzito’ huo, alionekana kusherehekea penzi lake na anayedaiwa kuwa mpenzi wake mwenye umri wa miaka 67.

“Wakiwachana na sisi ndio tunapendana,” Manzi wa Kibera aliandika chini ya picha ambayo alichapisha kwenye  mtandao wa Instagram.

Mrembo huyo aliyezingirwa na drama nyingi pia alishiriki video yake na mpenziwe wakiwa studioni wakionekana kurekodi kitu kama wimbo.

Hata hivyo, haijabainika iwapo mwanasosholaiti huyo mwenye utata ni mjamzito au anatafuta tu kiki  kama ilivyo kawaida ya wasanii wengi.

Haya yanajiri takriban miezi minne baada ya Manzi wa Kienra kudai kufanya harusi ya zaidi ya  shilingi milioni 6.8 na mzee huyo wake.

Katika mahojiano  na Mpasho, alisema kuwa harusi hiyo ilifanyika katika kiwanja kimoja cha kuchezea Gofu katika barabara ya Kiambu.

"Harusi tulifanya katika uwanja moja wa golfu katika barabara ya Kiambu lakini sitasema ni kiwanja gani hicho, tumeamua kuiweka iwe siri kati yangu na mpenzi wangu."

Mwanasosholaiti huyo alisema kuwa harusi hiyo ilikuwa na wageni 12 pekee na hawa walikuwa familia na marafiki wa karibu.

Mnamo mwezi Mei,Manzi wa Kibera alidaiwa kuvishwa pete ya uchumba na mzee huyo mwenye umri wa miaka 67.

Katika video zilizovuma kwenye mitandao ya kijamii, mwanasosholaiti huyo asiyepungukiwa na drama alionekana akiwa ameandamana na anayedaiwa kuwa mumewe kabla ya mzee huyo kupiga magoti na kumuomba wafunge ndoa. Makumi ya watazamaji kisha walisikika wakimtia moyo kukubali ombi hilo la ndoa.

"Sawa, nishasema ndio!" alisikika akimwambia mpenzi huyo wake baada ya muda mfupi wa kufikiria na kuzingatia.

Baada ya kukubali, mzee huyo aliyekuwa amevalia kapura nyeupe na koti nyeusi alionekana akimvisha pete ya uchumba.

Watazamaji waliweza kusikika wakimsihi mwanasosholaiti huyo kumbusu mchumba wake na  wanaonekana kutii ombi.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved