logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vera Sidika, Brown Mauzo waonyesha mtoto wao wa miezi 4 kwa mara ya kwanza

Vera na Mauzo wamemsherehekea mtoto wao mdogo, Prince Ice Brown anapotimiza umri wa miezi minne.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri06 July 2023 - 12:25

Muhtasari


•Vera Sidika alitumia fursa hiyo maalum kumuonyesha mwanawe kwa umma kwa mara ya kwanza tangu amzae.

•Brown Mauzo alimsherehekea mwanawe Ice Brown pamoja na watoto wake wengine wanne ambao ni Asia Brown, Lareesa Brown, Hakeem Mauzo na Zufla Brown.

wamemuonyesha mtoto wao kwa mara ya kwanza

Mwanasosholaiti Vera Sidika na mzazi mwenzake Brown Mauzo wamemsherehekea mtoto wao mdogo, Prince Ice Brown anapotimiza umri wa miezi minne.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 33 alitumia fursa hiyo maalum kumuonyesha mwanawe kwa umma kwa mara ya kwanza tangu amzae.

"Mwanangu @prince_icebrown ni mzuri sana, alinifanya nipagawe sana," Vera alisema kwenye picha yake akiwa amemshika mtoto huyo wake ambayo alichapisha kwenye mtandao wa Instagram.

Aliongeza, "Kheri ya miezi 4 ya kipenzi. Kubarizi nyumbani."

Mama huyo wa watoto wawili hata hivyo hakuonyesha sura kamili ya mvulana huyo lakini ni wazi kuwa ana ngozi nyeupe.

Brown Mauzo pia alisherehekea mwanawe huyo wa mwisho kuzaliwa pamoja na watoto wake wengine wanne ambao ni Asia Brown, Lareesa Brown, Hakeem Mauzo na Zufla Brown.

Vera Sidika na Mauzo walitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao Ice Brown mwishoni mwa mwezi Mei, takriban miezi mitatu baada ya kuzaliwa. Wakati huo, wawili hao walifichua kuwa  mtoto wao alizaliwa Machi 3, 2023.

Katika tangazo lake mnamo mwezi Machi, Vera alijigamba kwamba mwanawe, Ice Brown ndiye mvulana mzuri zaidi aliyewahi kuona.

"Kungoja kumekwisha! Mwana mfalme amezaliwa. Ice Brown, mvulana mzuri zaidi ambaye nimewahi kuona," alisema kwenye Instagram.

Aliambatanisha ujumbe wake na picha iiyomuonyesha akiwa hospitalini pamoja na mumewe na binti yao Asia Brown. Mwanawe mchanga alilazwa kwenye kitanda kidogo kilichowekwa kando ya kitanda chake cha hospitali

Brown Mauzo alitoa shukrani zake za dhati kwa Maulana kwa kumjalia yeye na mwanasosholaiti huyo mtoto wa pili pamoja.

"Ninashukuru sana kwa zawadi maalum Mungu ametubariki nayo. Tunakupenda kwa kutubariki kikamilifu. Maisha ni mazuri na wewe mvulana @prince_icebrown. Umeongeza maisha yetu kwa furaha na wakati mzuri. Asante kwa Mungu," Mauzo alisema.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved