logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zari akiri kutoka kimapenzi na Shakib kabla ya kuolewa na Diamond

Alikiri kwamba yeye na Shakib walichumbiana miaka kadhaa nyuma kabla ya kutengana na kurudiana

image
na Radio Jambo

Habari08 May 2023 - 05:48

Muhtasari


•Zari amedokeza alichumbiana na Shakib Cham kabla ya kujitosa kwenye ndoa na staa wa Bongo Diamond Platnumz.

•Zari alibainisha kuwa picha za Shakib na Ivan ambazo zimekuwa zikisambazwa zilipigwa wakati wakibarizi pamoja.

Mwanasosholaiti na mfanyibiashara maarufu kutoka Uganda Zari Hassan amedokeza kwamba alichumbiana na mume wake Shakib Cham Lutaaya kabla ya kujitosa kwenye ndoa na staa wa Bongo Diamond Platnumz.

Katika mahojiano ya hivi majuzi nchini Uganda, mama huyo wa watoto watano aliwathibitisha waandishi wa habari kwamba amemfahamu mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa miaka kadhaa sasa. 

Alikiri kwamba yeye na Shakib walichumbiana miaka kadhaa nyuma kabla ya kutengana na kurudiana tena mwaka jana.

"Nilichumbiana na Shakib huko nyuma kisha tukaenda njia tofauti. Sijui tulipatana vipi tena," Zari alisema.

Mzazi mwenza huyo wa Diamond Platnumz alisema haikuwa ngumu kuungana tena na Shakib na kufunga naye ndoa mwezi uliopita kwani waliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi katika siku za nyuma .

"Mwaka moja baada ya kurudiana alisema nitakufanya mke wangu. Ni hayo tu. Hatukuzungumza kwa muda kisha ghafla mwaka mmoja baada ya kurudiana tukafunga ndoa. Ikiwa sio Mungu, tutaiitaje hiyo?," alihoji.

Zari alirudiana na Shakib mapema mwaka jana baada ya kukatiza mahusiano na mfanyibiashara wa Uganda GK Choppa. Waliweka mahusiano yao siri hadi katikati mwa mwaka jana ambapo walifichua wanachumbiana.

Kumekuwa na tetesi nchini Uganda kuwa Shakib aliwahi kuwa mfanyikazi wa aliyekuwa mume wa Zari, marehemu Ivan Ssemwanga ikidaiwa kwamba hapo ndipo mahusiano yao yalipong'oa nanga. Katika siku za nyuma, picha za mfanyibiasha huyo wa miaka 31 akiwa pamoja na Ivan zilisambaa mitandaoni huku uvumi ukienezwa kuwa aliwahi kuwa mlinda lango kwenye makazi yake nchini Afrika Kusini.

Wakati akizungumza na wanahabari, Zari hata hivyo alizika tetesi hizo na kubainisha kuwa mumewe hakuwahi kuajiriwa na marehemu Ivan.

"Tunahitaji kuzungumzia hili. Nimeona watu wakisema kwamba Shakib alikuwa mlinzi wetu, eti aliwahi kufanya kazi kwa Ivan. Ili kuweka mambo wazi, Shakib hajawahi kufanya kazi kwa Ivan," Zari Hassan alisema.

Alibainisha kuwa picha za Shakib na Ivan ambazo zimekuwa zikisambazwa zilipigwa wakati wakibarizi pamoja.

Mwanasosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 42 aliamua kumwaga mtama baada ya mumewe kukwepa kuzungumzia madai hayo.

"Kila mtu yuko huru kusema anachotaka. Huwezi kuwazuia. Mimi najua ukweli. Yeye (Zari) pia anajua ukweli," Shakib alisema wakati alipoombwa kuzungumza kuhusu picha hizo na madai kuwa alikuwa mlinzi wa Ivan.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved