logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zari Hassan amzomea vikali shabiki aliyetapeliwa na mtu aliyejifanya yeye

Zari alibainisha kuwa hafahamu kabisa kile ambacho shabiki huyo alikuwa anazungumzia

image
na Radio Jambo

Habari30 October 2023 - 05:45

Muhtasari


•Zari Hassan amefichua mazungumzo yake na shabiki mmoja ambaye alitapeliwa maelfu ya pesa na mtu aliyemwiga.

•Shabiki huyo alitaka Zari amrudishie pesa zake kwa kuwa hakuwa amepokea R15,000 (Ksh 119,895) ambazo aliahidiwa.

Mwanasosholaiti na mfanyibiashara mashuhuri wa Uganda, ambaye anaishi Afrika Kusini, Zari Hassan amefichua mazungumzo yake na shabiki mmoja ambaye alitapeliwa maelfu ya pesa na mtu aliyemwiga.

Kulingana na screenshot iliyochapishwa na mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz, shabiki huyo alidai kuwa alimlaghai R3000 (Ksh 23,978) kwa ahadi kwamba angerudishiwa pesa hizo mara tano.

Shabiki huyo alikuwa amemtumia Zari ujumbe kwenye WhatsApp akitaka amrudishie pesa kwa kuwa hakuwa amepokea R15,000 (Ksh 119,895) ambazo aliahidiwa.

"Siku njema, tafadhali pesa yangu iko wapi? Sihitaji tena pesa yangu. Umesema nikilipa R3000 nitapokea R15,000 ndani ya siku 3, lakini hakuna kinachoonekana kwenye akaunti yangu,” shabiki huyo alimlalamikia Zari.

Aliendelea, “Tafadhali nitumie pesa zangu, nimemaliza kufanya hivyo. Nitumie tu R3k zangu. Nilikuambia kwamba nilikopa hiyo R3k ili kuanza uwekezaji na wewe na sasa unaomba pesa zingine. Tafadhali nirudishie pesa zangu.”

Katika majibu yake kwa shabiki huyo kwenye gumzo lao la WhatsApp, Zari alibainisha kuwa hafahamu kabisa alichokuwa anakizungumzia

Mfanyibiashara huyo aliendelea kumshauri arejee pale ‘dili la uwekezaji’ lilipoanzia akibainisha kuwa katika siku za nyuma aliwahi kuwaonya watu kuwa waangalifu na matapeli wanaofanya biashara mtandaoni kwa kutumia jina lake.

“Kwa kuanzia, sijui unaongea nini. Nakushauri urudi pale ilipoanzia ukamalizie hapo. Mbona nyie wapumbavu wote mnapoibiwa ndio mnapata namba au barua pepe hii,” Zari alijibu.

Aliongeza, "Mimi huwaonya watu kila siku kuhusu walaghai kwenye mtandao lakini nyote hamsikii. Tafadhali rudi pale ilipoanza na uombe urejeshewe pesa zako si hapa kwenye nambari hii. Sina biashara na wewe hata kidogo.”

Mwanasholaiti huyo mwenye umri wa miaka 43 alitangulia kumfahamisha shabiki huyo kwamba angeposti screenshot ya mazungumzo yao ili tu kuendelea kuwaonya watu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved