logo

NOW ON AIR

Listen in Live

PATANISHO: Wazazi Wamlazimisha Anthony Kumrudisha Mke Wa Zamani

PATANISHO: Wazazi Wamlazimisha Anthony Kumrudisha Mke Wa Zamani

image
na

Uchaguzi01 October 2020 - 16:09
patanisho
Hapo jana bwana Anthony aliomba apatanishwe na mkewe Nancy ambaye walikosana takriban mwaka mmoja uliopita. Naam mwaka mmoja.

Kulingana na Anthony, alikuwa na mpango wa kando jambo ambalo lilipelekea wawili hao kutengana na isitoshe, bwana huyu alipata mtoto na mwanamke huyo.

Kituko kilizuka wakti bwana huyu alifichua kuwa alikuwa na mipango ya kufanya harusi mwezi wa Disemba lakini mamake mzazi hampendi mwanadada huyo aliyewatenganisha Anthony na Lucy, kisa na maana ni mvivu na asiyeshughulikia mumewe.

"Mamangu aliniarifu kuwa hataki mwanadada huyo niliyekuwa na mpango wa kando naye, kwani ni mvivu na hamsaidii na kazi za nyumbani ikilinganishwa na Nancy ambaye ana bidii ya mchwa." Alijieleza Anthony.

Alipopigiwa simu, Nancy ambaye bado alikuwa usingizini alikataa katakata kurudiana na Anthony huku akiomba mda zaidi kufikiria.

Kulingana na Nancy, lazima wazazi wa Anthony wakazungumze na wazazi wake kabla yake kuamua, huku akifichua kuwa sio mpango wa kando tu uliowasambaratisha bali kuna mengi kama kutusiwa akiwa kwa ndoa.

Skiza kanda ifuatayo.

&feature=youtu.be


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved