logo

NOW ON AIR

Listen in Live

 Lamba Nyonyo? Wimbo mpya wa Willy Paul  wazua hamaki mtandaoni .

 Lamba Nyonyo? Wimbo mpya wa Willy Paul  wazua hamaki mtandaoni .

image
na

Burudani02 October 2020 - 02:46
Msanii wa muziki wa gospel Willy Paul yamkini  ameshazoea kejeli na  cheche za matusi makali ambayo hupokezwa mtandaoni .Hii ni kwa sababu nyota huyo  sasa hajali wanachosema watu akina yakhe kuhusu muziki wake kwa sababu licha ya kuimba nyimbo za kidini ,jina la wimbo wake mpya  ‘Lamba Nyonyo’ limesaliti kabisa msimamo wake . Pindi tu baada ya kuutundika wimbo huo mtandaoni ,wengi walionekana kukerwa na jina la wimbo huo na maneno ambayo yanaimbw ana Poze .

Baadhi ya watumizi wa mtandao wamemlaani kwa kuwahaibia sifa wasanii wengine wanaoimba gospel halisi  ingawaje kuna wachache ambao wanamtetea Willy Paul wakisema ana uhuru wa kuimba anavyotaka . Iwapo  unampebda Poze au nyimbo zake ,basi ‘Lamba nyonyo’ itakufanya uamue kukata uamuzi kumhusu  au kumkubali jinsi alivyo . Iwapo Willy Paul alichanganywa na Jina 'Lamba lolo' au 'Wamnyonyez' ni mungu pekee ajuaye kwa sababu yake  sasa yamegeuka mazito  and 'i gif up'!


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved