logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tecra Muigai bintiye mkurugenzi mkuu wa Keroche breweries aaga dunia

Tecra Muigai bintiye mkurugenzi mkuu wa Keroche breweries aaga dunia

image
na

Habari02 October 2020 - 09:24
Tecra

Tecra Muigai, binti yake mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Keroche breweries Tabitha Karanja amefariki katika ajali ya barabara.

Kulingana na taarifa ya kampuni hiyo, Tecra alifariki jana baada ya kuhusika katika ajali wakati wa mchana. Tecra ambaye alikuwa binti yake Tabitha na mwenyekiti wa Keroche Joseph Karanja alikuwa kiongozi wa mikakati na uvumbuzi katika kampuni hiyo.

Kwingineko, kaunti ya Mombasa imefutilia mbali gharama za wakaazi ambao walikuwa kwenye kwarantini. Katika taarifa iliyotolewa Jana, idara ya afya ya kaunti hiyo ilikubaliana na taasisi hiyo ya kutoa mafunzo ya udaktari na kuwachilia watu 38 ambao walikuwa wamewekwa kwenye kwarantini katika taasisi hiyo.

Hilo lilifanyika siku kadhaa baada ya wagonjwa kulalama kuwa kuwa hawawezi pata shilingi elfu ishirini na nane za kulipa taasisi hiyo baada ya mda wao wa kwarantini kutimia.

Hayo yakijiri, mwanaume mwenye umri wa miaka 30 amekamatwa katika kaunti ya Homa Bay kwa kumdhulumu kingono msichana mwenye umri wa miaka kumi anayeugua ugonjwa wa kifafa.

Mwanaume huyo alimdhulumu msichana huyo siku ya Ijumaa akiwa nyumbani kwao katika kijiji cha Otaro.

Inaripotiwa kuwa alijaribu kumshawishi msichana huyo wa gredi ya kwanza kwa kumpa shilingi 150 na kuamua kumfanyia unyama huo alipokataa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved