logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Nyanyangu alipata saratani wiki mbili baada ya kupoteza kazi yangu'-Jahmby Koikai asimulia

'Nyanyangu alipata saratani wiki mbili baada ya kupoteza kazi yangu'-Jahmby Koikai asimulia

image
na

Michezo02 October 2020 - 08:09
Huku wanahabari wa kampuni ya media max wakikumbana na masaibu ya kupoteza kazi zao Jahmby Koikai amewatia moyo kwa ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii na kuwataka wajipe moyo kwa maana Mungu ana mipango mingine mipya na ya ajabu.
"Nilikuwa najitayarisha kuzindua video mpya, nilipoteza kazi zangu zote mwaka wa 2015, nilikuwa nafanya kazi katika vituo viwili vya radio na kufanya kipindi kimoja katika runinga.

Nilikosa kipindi kimoja cha runinga kwa sababu ya maumivu ya hedhi, nilihakikisha waajiri wangu walijua maumivu yangu kwa hivyo nilikuwa napewa ruhusa ya siku saba kila mwezi.

Kuna wakati nilikosa kipindi kimoja lakini mtayarishi hakutaka kujua hali yangu, kwa hivyo nilifutwa kazi kwa ajili ya kukosa kipindi kimoja, muda huo wote sikufahamu nilikuwa na maradhi ya Endometriosis

Nilijaribu kutilia maanani kazi yangu ya redio lakini singeweza kwa maana afya yangu ilikuwa inazidi kudorora na kunifanya nyonge kutoweza kupanza ngazi.

Mazoea ya kampuni za habari kufuta watu kazi yalijiri na nikawa miongoni mwa watu 200 waliofutwa kazi, nilichukuwa barua yangu na kuelekea nyumbani." Alieleza Koikai.

Alizidi kunakili ujumbe wake na kusema,

"Huu ni msimu wa ajabu na mwema kuweni na imani, na muwe na matumaini mna talanta nyingi ambazo hazijulikani,shukuruni Mungu kwa ajili ya mitandao ya kijamii

Mnaweza kufanya kazi kupitia mitandao Mungu yupo katika kiti chake cha enzi na ana shughulikia hali yenu."

Chamno Koikai baada ya kufutwa kazi alikumbana na haya;

"Kama vile nyinyi nyote mwafahamu nililelewa na nyanya yangu na mama yangu wakati huo nilifutwa kazi nilienda nyumbani na kumpata nyanya yangu akiwa na maumivu ya tumbo.

Baada ya wiki mbili alipatikana na saratani ya kongosho, pia hali yangu ilikuwa inazidi kudhoofika nilipofanyiwa vipimo nilipatikana na Endometriosis.

Pia sauti yangu ilikuwa inazidi kupotea namshukuru @SELECTORTECHNIX ambaye alisimama na mimi hadi sasa.

Kwa miaka mitano sijakuwa katika kazi nzuri, nimepigana na hali ya afya yangu kwa muda hospitalini, nilirejea nyumbani mwaka jana ili kujiendeleza kimaisha lakini virusi vya covid-19 nikavuruga mipngo yangu lakini bado nina matumaini

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved