Kama huyajaona basi yapo njiani .ndio msemo pekee ambao sasa utakuacha na taswiraya mambo ya kutisha na hata kushangaza katika karne hii. Philis ameolewa na Eric na badala ya kuangazia masuala ya ndoa yake ameanza kutafakari iwapo kwa kweli alifanya kosa kuolewa na mwanamme …kisa na maana? Kwa sababu maajuzi amegundua kwamba huenda yeye ni mpenzi wa jinsia moja ama huenda yeye ni mtu wa kujihusisha katika mapenzi na jinsia zote mbili . Hajui lakini ni mojawapo kati ya hizo .
Sasa kuna haki kwa kila mtu kufanya anachotaka na maisha yake ya kimapenzi ,lakini haya ya Philis sasa yanashangaza kwa sababu anasema yeye an mpenda dadake mume wake yaani shemeji yake.
Sijui yatakuaje wakati mume wake atakapogundua kwamba mke wake na dadake wanafanya mambo ya pembeni ambayo yanatishia sio ndoa yake tu bali huenda ufichuzi huo ukaiuvunja familia yao kati kati!
Philis anasema wakati alipotambulishwa kwa shemeji yake ,hakuwa na hisia kwake lakini walipoanza kuzoeana na kufahamiana Zaidi alianza kuhisi kana kwamba walikuwa na mvuto Fulani kati yao . Walianza kuoga pamoja na shemeji yake na hata siku moja mambo yalizidi na wakapigana busu . Hapo ndipo mambo yalipochukua mkondo mwingine kwa sababu familia nzima ilifahamu kwamba shemeji yake alikuwa mpenzi wa jinsia mmoja na yeye tangia shule ya upili hajakuwa na mpenzi wa kiume . wengi walijua hilo lakini walijiambia labda ilikuwa hatua tu na wakati mmoja siku zijazo angerejesha fahamu zake na kuanza mahusiano na wanaume –Walikuwa wamekosea kwa sababu shemeji ya Philis hakuwa na mpango huo kwani sasa alikuwa ameanza kujitambulisha wazi kama msagaji . Ttaizo ni kwamba Philis naye kajipata katika lindi hilo la ushoga naye anasema kwa kweli hafahamu kilichotokea kwa sababu kufanya mapenzi na mume wake hakumpi furaha tena kama anavyoshiriki mapenzi na dada ya mume wake .
Amekuwa akifanya hivyo kisiri kwa muda lakini anafahamu hatari itakayolipuka endapo wanachofanya na shemeji yake yatagundulika . Makubwa haya hatujui yataisha vipi na muda ndio utakaosema kitakachotokea kwani kwa sasa ni ngoja ngoja ya kujua siku ambayo Eric atagundua kwamba mke wake amekuwa akipewa raha za kimapenzi na dadake!