Mtangazaji wa habari katika vituo vya Radio Africa Tina Mwambonu ameasi ukapera wikendi iliyopita baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Sam Ndirangu .
Tina ambaye husoma habari za kiingereza katika vituo vya Kiss na Classic pamoja na za Kiswahili katika kituo cha Radio Jambo amefurahia sana mwanzo wa awamu mpya katika maisha yake .
‘Kimekuwa kipindi kirefu cha kuingoja siku hiyo(ya harusi) na hatimaye inafanyika ,siwezi kungoja kuanza kuitwa mke wa Ndirangu’ alisema siku moja kabla ya siku yake ya harusi .
Miongoni mwa waliohudhuria harusi hiyo nio pamoja na watangazaji wenzake wa RAL , Tina Masika na Afrikan Njogu na Andrew Lucheli
Harusi hiyo ya waalikwa pekee ilifanyika huko Nakuru na hapa tunakuvurumishia picha kadhaa za hafla hiyo .