Samu Mbuvi mapema wiki alivuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufichua kwamba seneta wa Lamu Anwar ambaye ni baba wa mtoto wake kwamba amekuwa akimdhulumu katika uhusiano wao.
Kupita kwenye ukurasa wake wa instagram Saumu alipakia picha akionyesha majeraha kwenye uso wake na kudai kwamba alikuwa amechapwa na seneta huyo.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alisema kwamba baadhi ya wanaume hawajui bei ya 'pampers' ilhali wanajua kuongea kama wanawake.
"KIla mwanamke anaweza kuwa mama lakini inagharimu mama mbaya kuwa baba, hamjui bei ya pampers lakini mnapiga kelele kama mwanamke," Aliandika Saumu.
Seneta huyo akiwa kwenye mahojiano na mpasho alikiri kwamba alimchapa Saumu mara moja kabla ya kujua kama ana shida ya akili.