Katika kila kona za nchi, na kama wewe nimwanadamu lazima kuna kikundi au watu ambao wanapenda kuzungumzia maisha yako na hata kuingilia maisha yako.
Kuna baadhi ambao hurudi na nyuma kwa ajili ya maneno ya watu, na wale ambao ukabiliana nao ipasavyo na kuwapa kikomo.
Je wafahamu njia zozote za kukabiliana na watu ambao wanaingilia maisha yako, na kuchunguza kile unaendeleza katika maisha yako?
Haya basi usitie shaka, hizi hapa njia za kukabiliana na watu kama hao.
1.Jaribu kuchunguza kama wanakutakia mazuri
Kuna wale watu wataingilia maisha yako wakitaka mazuri yakutendekee lakini kuna wale wanataka kukuangamiza milele na kukuona ukilia kila kuchao.
Kama hawakutakii mazuri haya basi jipe shughuli.
2.Weka mipaka
Kuna baadhi ya watu na marafiki ambao hawafahamu wala kujua mipaka katika maisha yako, kuna wale watavuka mipaka na kukuumiza.
Kama una marafiki usiweze kuzungumza na mtu mwingine kuhusu maisha ya rafiki mwenzake weka mipaka na ukatae maneno yake kwa maana yataleta chuki siku moja.
3.Wapuuze
Kuna watu wengine ambao huwezi kuwazuia na lazima udumishe uhusiano wa kiraia nao, kama mwenzako au jirani yako. Ikiwa wataingilia maisha yako, labda ni bora usiwape maanani.
4.Usiwaambie siri zako
Maelezo yako ya kibinafsi huchochea watu wenye ujinga, kwa sababu mara tu watakapojua kitu kukuhusu watataka kutoa maoni juu yake au kuuliza. Kwa hivyo jaribu kuweka mambo ya kwako, hata ikiwa watakuuliza juu yake nyamaza.
Kuna wale wazee ambao watakuuliza kwanini hujaoa au kuolewa nyamaza na ufanye mambo yako kisiri.