logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Uteuzi wa kocha mpya wa timu ya soka ya Harambee Stars wazua gumzo mitandaoni

Baadhi ya Wakenya wameeleza wasiwasi wao kuhusiana na matokeo hafifu ambayo kocha Firat ameandikisha na timu ambazo amekuwa akisimamia hapo awali

image
na Samuel Maina

Michezo20 September 2021 - 10:18

Muhtasari


  • •Wakenya wamekuwa wakitumia mitandao wa kijamii ya Twitter kuelezea kutoridhishwa kwao na uteuzi wa mkufunzi mpya wa timu ya taifa ya soka Harambe stars Mturuki Engin Farat.
  • •Baadhi ya Wakenya wameeleza wasiwasi wao kuhusiana na matokeo hafifu ambayo kocha Firat ameandikisha na timu ambazo amekuwa akisimamia hapo awali
Engin Firat

Uteuzi wa kocha mpya wa timu ya taifa ya soka Kenya umezua gumzo mitandaoni.

Wakenya wamekuwa wakitumia mitandao wa kijamii ya Twitter kuelezea kutoridhishwa kwao na uteuzi wa mkufunzi mpya wa timu ya taifa ya soka Harambe stars Mturuki Engin Farat.

Shirikisho la Soka la nchini Kenya (FKF) lilitangaza uteuzi wake Siku ya Jumapili kwa kandarasi ya miezi miwili.

Baadhi ya wakenya wamekuwa wakihoji jinsi Mkuu wa FKF Nick Mwendwa alivyoafikia uteuzi huo.

Baadhi yao wameeleza wasiwasi wao kuhusiana na matokeo hafifu ambayo kocha Firat ameandikisha na timu ambazo amekuwa akisimamia hapo awali

Firat anachukua nafasi ya Jacob 'Ghost' Mulee ambaye alijiuzulu wadhifa huo siku chache zilizopita.

Mtumiaji mwingine wa mtandao huo JG anamtetea Nick Mwendwa akisema amejitahidi kadri ya uwezo wake kutatua matatizo ambayi yamekua yakiikabili Harambee Stars kwa miaka kadhaa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved