Je wajua kwamba mwanafunzi ambaye kwa sasa yuko katika darasa la saba atakuwa katika kidato cha kwanza mwezi Januari mwaka ujao? , kama hujui basi habari ndio hiyo.
Janga la corona liliathiri mfumo wa elimu hapa nchini Kenya huku wizara ya elimu na serikali kwa ujumla zikilazimika kutafuta mbinu mbadala ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanamaliza masomo yao kwa wakati uliokusudiwa.
Wizara ya elimu ilitoa kalenda na tarehe rasmi za masomo mwaka huu wa 2022/2023, huku wanafunzi wakitarajiwa kusonga katika darasa lifuatalo. Lakini swali kuu ni je, wazazi wako tayari kugharamikia karo katika kipindi hicho?
Muhula wa kwanza ambao utadumu kwa wiki 10 utaanza rasmi tarehe 25/04/2022 mpaka tarehe 1/7/2022, huku wanafunzi hao wakitarajiwa kusonga katika madarasa tofauti ifuatavyo:
- Darasa la nane wataingia kidato cha kwanza
- Darasa la saba wataingia darasa la nane
- Darasa la sita wataingia darasa la saba
- Gredi ya tano wataingia gredi ya sita
- Gredi ya nne wataingia gredi ya tano
- Gredi ya tatu wataingia gredi ya nne
- Gredi ya pili wataingia gredi ya tatu
- Gredi ya kwanza wataingia gredi ya pili
- Pp2 wataingia gredi ya kwanza
- PP1 wataingia PP2
- Play school wataingia PP1
Muhula wa pili nao utang’oa nanga tarehe 11/07/2022 hadi tarehe 16/9/2022 na pia kudumu kwa wiki kumi.
Muhula wa tatu ambao kwa kawaida huwa mfupi, utadumu kwa wiki tisa pekee huku ukitarajiwa kuanza tarehe 26/9/2022 na kumalizika 25/11/2022.
Wanafunzi walio katika darasa la saba kwa sasa, watafanya mtihani wao wa kitaifa {darasa la nane} tarehe 28/11/2022 na kutamatisha tarehe 1/12/2022.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa wanafunzi walio katika gredi ya tano kufanya mitihani yao ya CBC almaarufu KCBE, huu ukiwa ni mfumo mpya unaolenga kuboresha vipaji vingine zaidi vya wanafunzi kando na masomo.
Inaaminika kwamba mwaka kesho, 2023 chini ya miezi kumi na mmoja kalenda ya masomo itakuwa isharejea katika ukawaida wake na wanafunzi watasonga katika madarasa yafuatayo:
- Wanafunzi walio katika darasa la nane kwa sasa watakuwa katika kidato cha pili
- Wanafunzi walio katika darasa la saba watakuwa katika kidato cha kwanza
- Wale walio katika darasa la sita wataingia darasa la nane na kufanya mtihani wa kitaifa [KCPE] mwaka uohuo.
- Wanafunzi katika gredi ya tano watakuwa wameingia gredi ya saba [junior secondary school]
- Walio katika gredi ya nne watakuwa wameingia gredi ya sita na kufanya mtihani wa KCBE mwishoni mwa mwaka wa 2023
- Wanafunzi walio katika gredi ya tatu watakuwa wameingia gredi ya tano
- Wale walio katika gredi ya plili kwa sasa watakuwa katika gredi ya nne
- Na wale walio katika gredi ya kwanza watakuwa katika gredi ya tatu
- Waliopo katika PP2 kwa sasa watakuwa wamesonga hadi gredi ya pili
- Wanafunzi katika PP1 watakuwa wameingia gredi ya kwanza
- Huku wale waliopo katika play school kwa sasa wakiingia PP2 wakati huo
Wazazi ambao wanao wapo katika darasa la saba kwa sasa, wanaombwa kufahamu kwamba itimiapo mwezi Januari mwaka 2023 wanafunzi hao watakuwa katika kidato cha kwanza na wale waliopo katika katika gredi ya tano wakitarajiwa kuwa katika junior secondary huku kitendawili cha ulipaji karo kikizidi kuzua hali ya tata ikifahamika kwamba wazazi wengi wamepitia kipindi kigumu tangu janga la Corona liingie katika taifa letu.
Sawia na mwaka jana, huu utakuwa mwaka wenye vipindi vifupi vya mapumziko kwa wanafunzi kando na likizo ya mwezi Aprili ambayo inatarajiwa kuwa ndefu zaidi.