logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond Platnumz na Wema Sepetu watambuliwa kama wapenzi bora wa zamani

Diamond alitoa shukrani kwa Wema na kuwasihi wengine kuhifadhi uhusiano mwema hata baada ya kutengana.

image
na Radio Jambo

Football17 February 2022 - 03:00

Muhtasari


•Diamond Platnumz na mwigizaji Wema Sepetu waliweza kushinda tuzo la wapenzi bora  wa zamani kutokana na uhusiano wao mwema baada ya kutengana.

•Diamond alitoa shukrani kwa Wema huku akiwasihi wapenzi wengine kuhifadhi uhusiano mwema hata baada ya kutengana.

Wiki hii imekuwa wiki maalum kwa wapendanao na imetukumbusha kuhusu watu maalum katika maisha yetu.

Je, Ex ana umuhimu upi katika maisha yako na uhusiano wako naye unapaswa kuwaje baada ya kuachana? 

Mapema wiki hii kwenye hafla ya Mahaba Ndi Ndi Ndi iliyoandaliwa katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dares Salaam, Tanzania kulipeanwa tuzo mbalimbali kwa wapenzi mashuhuri wa sasa na wa zamani.

Staa wa Bongoflava Diamond Platnumz na mwigizaji Wema Sepetu waliweza kushinda tuzo la wapenzi wa zamani bora kutokana na uhusiano wao baada ya kutengana.

Wapenzi hao wawili wa zamani walishinda tuzo hilo kwa mujibu wa kura za mashabiki waliohudhuria tamasha hiyo iliyoandaliwa usiku wa Valentine's.

Diamond pekee ndiye aliyepokea tuzo hilo kwani Wema Sepetu  mwenyewe hakuonekana kwenye hafla hiyo.

Baba huyo wa watoto wanne wanaojulikana alitoa shukrani kwa Wema huku akiwasihi wapenzi wengine kuhifadhi uhusiano mwema hata baada ya kutengana.

"Kwanza namshukuru ex mwenzangu. Pia natoa ujumbe kwa ndugu zangu wengine, tunapotengana tukae kwa amani. Nashukuru" Diamond alisema.

Diamond alikabidhiwa tuzo hilo na msemaji wa Young Sports Haji Manara.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved