Mwanamuziki Arrow Bwoy ametangaza wazi kuwa hatawahi kutumia kiki kupeleka mbele muziki wake ambao unaendelea kuimalika kila uchao.
Amesema kuwa chochote asemacho kwenye mitandao ya kijamii na katika mahojiano huwa cha kweli na sio kiki.
Mpenzi huyo wa Nadia Mukami ameapa kutotumia njia za mkato kukuza muziki wake kama wafanyavyo wasanii wengine wa hapa nchini
"Kwa wale wanaofanya kiki labda inawafanyia kazi .lakini kama Arrow Bwoy, watu watashabikia muziki wangu hata bila kiki yoyote, Kiki haijawai kunifanyia kazi. Ukiona kitu au nikiposti kitu,fahamu ni kweli . nitakuwa nikifanya hivyo kutoka ndani ya moyo wangu," Alisema Arrow Bwoy.
Hivi majuzi, mwimbaji huyo alitembelea mitaa ya mabanda ambapo aliwanunulia chakula mashabiki wake. Alidai kuwa hana uhakika kuhusu kiasi cha fedha ambacho alitumia siku hiyo.
Arrow Bwoy aliwashukuru mashabiki wake huku akieleza kuwa wamekuwa wakimuunga mkono tangu alipojitosa kwenye tasnia ya muziki.
"Nilifurahia sana kujumuika na mashabiki, nilirudi nyumbani nikiwa na hisia mingi, kwa Pesa nilizotumia kununua. Niliweka tabasamu kwa watu. nyuso na siwezi kuweka bei kusaidia."