logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanaume, 56, ajikata nyeti kwa kutumia kisu cha jikoni

Nakuru: Mwanaume ajikata korodani kwa kutumia kisu cha jikoni.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri20 April 2022 - 08:24

Muhtasari


• Mwanaume mmoja mjini Nakuru amekata korodani zake kwa kutumia kisu cha jikoni katika jaribio la kujitoa uhai.

Wataalam wa upasuaji katika chumba cha upasuaji wakimshughulikia mgonjwa

Mwanaume mmoja mjini Nakuru amekata korodani zake kwa kutumia kisu cha jikoni katika jaribio la kujitoa uhai.

Kulingana na ripoti ya polisi waliofika kwenye eneo la mkasa, Waweru Njoroge mwenye umri wa miaka 56 alivizia jikoni na kuchukua kisu kujikata korodani zake wakati mke wake alikuwa anakoga bafuni.

Kwa bahati nzuri mkewe alisikia usiahi mkali kutoka na mwanaume huyo aliyekuwa akiungulia machungu ya kitendo chake na kwa usaidizi wa wahisani wema walimkimbiza hospitalini ambapo hali yake ilidhibitiwa.

Mwanaume huyo bado hajapata ufahamu dhabiti wa kuelezea polisi kiini cha kufanya kitendo hicho cha kujeruhi nyeti zake.

Katika siku za hivi karibuni tangu ujio wa janga la Corona, kumekuwa na mripuko mkubwa wa watu wanaojitoa uhai kwa njia mbalimbali tena za kushangaza.

Baadhi wanahisi wengi wametamauka na gharama ya juu ya maisha na bei ya bidhaa mbalimbali nchini ikiendelea kukwea mlima na kazi za wengi kukatika kutokana na makampuni mengi kupunguza wafanyakazi kwa kukosa faida ambapo uchumi ulilemazwa pakubwa na virusi hivyo vya covid-19.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved