logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ujumbe wa DP Ruto kwa Isaac Rutto baada ya kumpoteza mama yake

Mamake Isaac Ruto alifariki Jumanne asubuhi katika hospitali ya MTRH

image
na Radio Jambo

Burudani15 June 2022 - 10:07

Muhtasari


  • Naibu Rais William Ruto ametuma rambirambi zake kwa Isaac Ruto, kiongozi wa chama cha CCM
Naibu rais William Ruto

Naibu Rais William Ruto ametuma rambirambi zake kwa Isaac Ruto, kiongozi wa chama cha CCM.

Ruto alimfariji gavana huyo wa zamani huku akimuomboleza mama yake na hata kunukuu mstari wa biblia kutoka kitabu cha  Zaburi 147:3 .

"Mungu ampe aliyekuwa Gavana wa Bomet Isaac Rutto nguvu za kustahimili kifo cha mama yake mpendwa, Jane Tirop. Ufarijiwe na neno la Bwana katika Zaburi 147:3: "Yeye huwaponya waliovunjika moyo, na kuzifunga jeraha zao. ”, DP Ruto alisema.

Mamake Isaac Ruto alifariki Jumanne asubuhi katika hospitali ya MTRH, alikokuwa akipokea matibabu.

Habari za kifo chake zimesitisha kampeni zilizokuwa zikifikia kiwango cha juu katika Kaunti ya Bomet.

Viongozi wengine ambao wametuma rambirambi zao kwa kiongozi huyo wa chama cha CCM ni pamoja na Hillary Barchok aliyemaliza muda wake na Hillary Sigei, mgombea useneta kwa tiketi ya UDA kaunti ya Bomet. Kifo cha Jane Tirop kiliwakusanya wote, na kuzika tofauti zao za kisiasa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved