Je, unajua kwamba unaweza kutumia Airtel Money katika maisha yako ya kila siku katika mitandao yote bila shida? Kadi yako ya Simu ya Airtel inaleta urahisi katika maisha yako. Kwa nini kutumia zaidi kwenye ada ya manunuzi wakati unaweza kuokoa zaidi na Airtel Money?
Faida za Airtel Money
1. Till ni Till
Unaweza kulipia bidhaa kwenye tills nyinginezo ikiwemo M-PESA bila kutozwa ada yoyote. Unapotaka kulipa ama kulipia bidhaa kwenye M-PESA till, unachotakiwa kufanya ni kubonyeza *222# alafu uchague nambari 6 au utumie App ya Airtel na kisha uchague kununua bidhaa. Utaarifiwa kupitia ujumbe wa manunuzi wa Airtel Money, na mfanyabiashara atapokea pesa mara moja.
2. Tuma Pesa kwenye mitandao (Airtel kwa Airtel FREE)
Wateja wanaotumia Airtel Money wanaweza kutuma pesa kwa gharama nafuu kupitia mitandao mbalimbali. Hata hivyo, ni bure wakati wanapotuma pesa kwa wateja wengine wa Airtel. Unachohitajika kufanya ni kubonyeza*222# na uchague tuma pesa au utumie App ya Airtel. Kwa hiyo kama wewe na mpendwa wako wote mnatumia Airtel Money, unapata akiba kwa gharama za manunuzi na kutumia akiba unayofanya ili kuongeza muda wako wa maongezi au kununua data. Kila shilingi unayohifadhi kwa gharama za manunuzi inaweza kwenda kwa matumizi makubwa. Fikiria juu yake, ni mara ngapi unaondoa pesa kutoka kwa mkoba wako wa rununu? Kumbuka haba na haba hujaza kibaba, ukifanya haya yote utaongeza akiba ya ajabu.
3. Akiba ya hadi 40% kwa malipo ya uondoaji.
Wateja wa Airtel Money wanaokoa hadi asilimia 40 kwa gharama za manunuzi, wanapotoa pesa kwa kutumia Airtel Money. Ili kutoa pesa, wateja hupiga *222# na kuchagua kutoa Pesa au wanatumia App yangu ya Airtel na kuchagua Toa Pesa.
4. Unaweza pia kufurahia malipo ya sifuri kwenye malipo ya bili ya matumizi
Kwa kushirikiana na Airtel Money, wateja wanafurahia malipo ya bure kwa huduma za maji, umeme na Pay TV kama DSTV, GOtv na Zuku. Ili kulipia bili hizi wanapiga *222#, chaguo 6 kisha Airtel Paybill au kupitia App ya Airtel kisha chagua Paybill.
iIli kuongeza pochi yako ya Airtel Money, unaweza kuhamisha pesa kutoka kwa akaunti yako ya benki, kutoka kwa wakala wa Airtel Money au kutoka dukani. Pata laini yako ya Airtel leo ili upate uzoefu wa akiba kwa wingi kwenye Airtel Money.
Airtel Money. Instant. Secure. Borderless.