logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Harmonize hatobadili dini kwa sababu ya ndoa!" Mwijaku ameweka wazi

"Mwijaku mimi siwezi kubadili dini mimi ni muislamu na nitaemdelea kuwa muislamu na ikitokea nikitangulia mbele ya haki nitazikwa kiislamu" Harmonize alimwambia.

image
na Radio Jambo

Michezo29 June 2022 - 12:49

Muhtasari


• "Kwa kauli yake yeye mwenyewe amenaminia kua hawezi kubadili dini na yeye bado ni muislamu" - Mwijaku

• Mwijaku pia alielezea kwamba msanii huyo hana lengo la kumshrutisha mkewe mtarajiwa Fridah Kajala Masanja kubadili dini ili kuwa muislamu.

Mtangazaji mwenye utashi mkubwa kutokea shirika la habari la Clouds nchini Tanzania, Mwijaku amewaondoa mashabiki wa bosi wa Konde Music Worldwide Harmonize kwamba msanii huyo hana nia yoyote ya kubadili dini haswa baada ya kumvisha mwanasosholaiti kajala Masanja pete ya uchumba.

Mwijaku ambaye amejibatiza kwa jina la DC wa Instagram kwa muda mrefu ameshindwa kueleweka machoni pa wengi kwa vile anaonekana kuwa upande wa Harmonize sana huku akimpiga vijembe vya chini kwa chini mbaya wake kimuziki, Diamond Platnumz hali ya kuwa anaramba dili za ubalozi kama vile Wasafi bet.

Kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakipelekana mbio na mtaalam wa ujenzi wa majumba ambaye pia ni mwanamuziki Baba Levo kila mmoja akionekana kuwa kama chawa vile kwa kuvuta upande wa yule anayempiga sapoti – Mwijaku akivuta zaidi upande wa Harmonize naye Baba Levo akivuta kwingi upande wa Diamond Platnumz.

Mwijaku ameandika kwenye Instagram yake kwamba Harmonize ambaye ni Muislamu hatobadili dini kwa sababu ya penzi la Kajala.

“Niwaondoe shaka waislamu na wale ambao sio waislamu. Kuhusu DINI na kuhuhusu KUBADILI dini kwa msanii @harmonize_tz. Nilipata bahati kuongea nae juu ya swala hili haraka tu baada ya kuona clip ya yeye akionyesha ishara ya msalaba. Kwa kauli yake yeye mwenyewe amenaminia kua hawezi kubadili dini na yeye bado ni muislamu na chochote kitakacho tokea hakiondoi imani yake ya kiislamu. Mambo ya mitandao tu video clip ni sehemu ya ishara kua bado yupo pamoja na watu woote na wenye dini zoote pasi na kubagua,” aliandika Mwijaku.

Kwa vile wengi wanamchukulia mtangazaji huyo kimzaha tu ilibidi azidi kusema zaidi na mpaka kunukuu maneno ya Harmonize alipomuuliza kuhusu kubadili ndoa ili kuwa mkristo kwa ajili ya kuokoa huba lake na Kajala.

“Kauli ya @harmonize_tz kwangu . MWIJAKU MIMI SIWEZI KUBADILI DINI MIMI NI MUISLAMU NA NITAEMDELEA KUWA MUISLAMU NA IKITOKEA NIKITANGULIA MBELE YA HAKI NITAZIKWA KIISLAMU. NA SITA HARIBU IMANI YA MTU KWA MATAKWA YANGU ILA NARUHUSU USHAWISH KWA MATAKWA YA ALLAH. @kajalafrida ATAKUA MKE WANGU NA SITAMFOSI KUBADILI DINI. IMANI YANGUNA IMANI YA MKE WANGU MTARAJIWA ZITABAKIA KAMA ZILIVYO NA MUMGU NDIO MUWEZA NA MUAMUZI YA HATMA YA MKE WANGU MTARAJIWA KWANGU. DC - NAKUHAKIKISHIA KUA SITABADILI DINI YANGU YA KIISLAMU NITAISHI KWA UNYENYEKEVU NA MALEZI NILIO PEWA WAZAZI WANGU YA KIISLAMU KWANGU,” Mwijaku alimnukuu Harmonize.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved