logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Aden Duale wa UDA Ashinda Ubunge Garissa Township Kwa Mara ya 4 Mtawalia

Mbunge huyo, mfuasi shupavu wa DP William Ruto na aliyekuwa kiongozi wa wengi alipata kura 9,905 dhidi ya kura 5,972 za Nasir Dolal

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku11 August 2022 - 08:46

Muhtasari


• Wengine ambao Duale alikuwa anamenyana nao katika kinyang’anyiro hicho ni pamoja na Abdullahi Mohamed wa UPIA aliyepata 5,529.

Aden Duale, mbunge wa Garissa Mjini akisherehekea ushindi

Mbunge wa muda mrefu wa Garissa Mjini Aden Duale ametangazwa kuwa mshindi waceneo bunge hilo kwa mara ya nne mfululizo kupitia chama cha UDA huku akimbwaga mshindani wake wa karibu Nasir Dolal aliyekuwa anamtoa kijasho kupitia chama cha ODM.

Mbunge huyo, mfuasi shupavu wa DP William Ruto na aliyekuwa kiongozi wa wengi alipata kura 9,905 dhidi ya kura 5,972 za Nasir.

Mapema mwaka jana Duale baada ya kung’atuliwa katika wadhfa wake wa kuwa kiongozi wa wengi kwenye bunge la kitaifa kwa kuegemea mrengo wa naibu rais William Ruto alitangqaza kwamba hangewania tena ubunge bali jukumu lake kuu lilikuwa ni kuhakikisha anampigia debe naibu rais Ruto ili atakaposhinda yeye atapata nafasi ya kujivinjari kwenye ikulu kifahari akinywa chai.

Duale aling’atuliwa katika mageuzi ambayo yalionekana kuwa ni mabadiliko rais Kenyatta alikuwa anafanya kwa kuwaangushia shoka la ghadhabu wabunge na viongozi waliokuwa wanaegemea mrengo wa naibu rais jambo lililotishia kusambaratika kwa chama cha Jubilee.

Nafasi yake ilikabidhiwa mbunge anayeondoka wa Kipipiri Amos Kimunya ambaye pia jana ametangaza kukubali kushindwa katika jaribio lake la kutaka kuwa mbunge wa eneo hilo kwa mara ya nne mfululizo pia kama Duale.

Wengine ambao Duale alikuwa anamenyana nao katika kinyang’anyiro hicho ni pamoja na Abdullahi Mohamed wa UPIA aliyepata 5,529 na kumaliza nambari tatu na Siyad Osman alipata kura 952 akifunga nne bora.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved