logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kutokana na shinikizo kutoka kwa umma, wiki ijayo nampachika mimba mke wangu - Terence Creative

Mimi nimejitolea kuwawekea kamera bila malipo. Tunahitaji kurekodiwa tukio hili kubwa - DJ Mo alimtania.

image
na Radio Jambo

Michezo12 October 2022 - 07:34

Muhtasari


• Miezi michache iliyopita, Terence na mkewe Milly Chebby walisherehekea miaka 10 katika ndoa.

Terence asema atampa mkewe mimba wiki kesho

Mchekeshaji na muigizaji maarufu wa humu nchini Lawrence Macharia almaarufu Terence Creative amezua gumzo mitandaoni baada ya kuweka wazi kwamba anapata shinikizo la kumpa mimba mkewe kutoka kwa umma – mashabiki wake.

Kupitia kurasa zake za mitandaoni, tangu siku ya Jumanne familia ya wanamuziki Wahu na Nameless kutangaza kupokea mtoto wao wa tatu ambaye nib inti, Terence amekuwa akiwahongera huku akizua utani kuhusu Baraka hiyo yao mpya katika familia.

Alisema kwamba kutokana na shinikizo hilo kutoka kwa umma, wiki kesho atahakikisha anampa mimba mkewe, Milly Chebby.

“Kutokana na shinikizo na takwa kutoka kwa umma, wiki kesho nitampa mimba mke wangu,” Terence Creative aliandika.

Mashabiki wake pamoja pia na wanablogu na watu maarufu wenzake walifurika kwenye chapisho hilo na kuzua utani mkali huku wengine wakimwambia kwamba wangependa kurekodiwa tukio hilo na kushuhudia baadae.

“Mimi nimejitolea kuwawekea kamera bila malipo. Tunahitaji kurekodiwa tukio hili kubwa,” mcheza santuri maarufu DJ Mo alimtania.

Awali akimhongera Nameless kwa kumkaribisha mgeni mpya kwenye familia yake, alisema kuwa angekuwa ni yeye angerekodi matukio hayo yote na kuyaachia kwa njia ya vipindi kila tukio moja likiwa na sehemu yake. Nameless pia alipata kujibu mipigo katika tangazo hili la Terence kwa kumuuliza kwamba atatoa vipindi vingapi.

“Halafu utoe vipindi vingapi mkuza maudhui wangu?” Nameless alimtania.

“Umesema ni muhimu junior apate mtu wa kucheza naye wakati unacheza na mama yake,” msanii MTU alimuuliza.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved