Muigizaji maarufu Jackie Matubia amekuwa hospitalini kwa muda ambao haujathibitishwa.
Matubia alitangaza habari hizo na mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Alhamisi asubuhi ambapo alibainisha kuwa amekuwa mgonjwa kwa siku kadhaa. Kuthibitisha hayo, alichapisha picha yake akiwa amelala katika kitanda cha hospitali.
Katika picha aliyochapisha, mama huyo wa watoto wawili alionekana akiwa ameunganishwa kwenye kifaa cha kupima shinikizo la damu. Pia alikuwa na sindano kwenye mkono wake wa kushoto.
Hata hivyo, hakufichua maelezo zaidi kuhusu ugonjwa unaomuathiri.
"Kwa afya njema! Nimekuwa na siku chache mbaya zaidi," aliandika kwenye Instastori zake.
Muigizaji huyo hata hivyo aliendelea kuchapisha video zingine kwenye Instastori zikimuonyesha akifanya matangazo ya bidha mbalimbali. Muda ambao video hizo zilirekodiwa hata hivyo haujabainishwa.
Matubia na mchumba wake Blessing Lung’aho walimkaribisha duniani mtoto wa kiume takriban miezi sita iliyopita.
Matubia alitumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza kuwasili kwa mwanawe akimshukuru Mungu kwa kujifungua salama.
Wanandoa hao walichapisha picha wakiwa na mtoto wao katika hospitali na kuandika;
"Habari ya asubuhi☺️Habari njema!!! Hatimaye mtoto amefika!!! Tunamshukuru Mungu kwa kujifungua salama.. Asante, familia kwa maombi yenu. Jumatatu Njema!"
Matubia ni mama wa watoto wawili kwa kuwa ana mtoto wa kike kutoka kwa uhusiano wake wa hapo awali.
Mwishoni mwa Novemba, Matubia alitangaza kuwa amefanyiwa utaratibu wa kupunguza uzito kwa kuwekwa puto ya Allurion kwenye tumbo lake.
"Inchi zinaingia kwa muda wa miezi 2 na Baloon ya Allurion na nimesonga kutoka kilo 105 hadi sasa kilo 93.3. Mtazamo bora zaidi unakuja baada ya kupanda kugumu zaidi," alisema.
Matubia alisema utaratibu huo ulichukua dakika 15 pekee na ulimgharimu takriban Sh500,000.