Taasisi ya magonjwa ya Moyo nchini Tanzania ya Jakaya Kikwete imeshauri jamii kwamba kunywa angalau bia tatu kwa siku ili kuzuia magonjwa ya moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dk Peter Kisenge amesema hayo Jumatatu Julai 10, 2023 katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).
Amesema kuna wagonjwa wa moyo nchini.
"Asilimia kubwa ya wanaolazwa hospitali ni wagonjwa wa moyo na shinikizo la damu," aliambia vyombo vya habari.
Dk Kisenge alishauri kufikiria kula lishe bora hasa mboga za majani na matunda, matunda vyakula vya wanga na sukari.
“Unywaji bia, angalau mnywaji anywe bia tatu kwa siku,” alishauri, kama alivyonukuliwa na Mwananchi.
Kando na hayo, daktari huyo pia aliwashauri watu kuwa na mazoea ya kuangaliwa afya zao mara kwa mara ili kubaini matatizo katika mfumo wa mwili yqa kuyatafutia suluhu mapema.
Tamko hili la watu kunywa pombe angalau kwa siku linakuja wiki chache tu baada ya utafiti mwingine uliochapishwa na CNN pia kuwiana nao kwamba watu ambao wanakunywa pombe kwa kiasi cha wastani huwa wana viwango vya chini vya magonjwa ya moyo, unyongovu na msongo wa mawazo.
Dk. Ahmed Tawakol, mwandishi mkuu wa utafiti na mkurugenzi-mwenza wa Kituo cha Utafiti wa Picha za Moyo na Mishipa katika Hospitali Kuu ya Massachusetts, alibainisha kuwa baada ya kunywa pombe kidogo, kabla ya kuhisi kulewa, unahisi utulivu.
