logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mjane wa aliyepanga shambulizi la Dusit anaishi katika mazingira duni nchini Somalia, idara za usalama zasema

Mjane kisha aliolewa na kamanda aliyeuawa wakati wa makabiliano na Jeshi la Taifa la Somalia.

image
na

Yanayojiri17 January 2024 - 10:18

Muhtasari


• Mwanahabari huyo aliyegeuka kuwa mfuasi wa kundi la kigaidi alikuwa mke wa Ali Salim Gichunge ambaye alitekeleza shambulio la kigaidi kwenye jumba la  DusitD2.

Violet Kemunto Omwoyo. Picha: HISANI

Miaka mitano baada ya mumewe kuuawa katika shambulizi la DusitD2 jijini Nairobi, Violet Kemunto Omwoyo anaishi katika maisha duni nchini Somalia, yanayodhihirisha maisha duni ya vijana wanaoshawishiwa kuingia katika makundi ya kigaidi na yenye misimamo mikali ya kidini.

Kulingana na maelezo ya kijasusi, maisha hayajakuwa mazuri kwake, huku akizungushwa kutoka kwa mume mmoja mpiganaji hadi mwingine, na ni bahati tu inaweza kuelezea kwa nini hajauawa.

Huku nchi ikiadhimisha miaka mitano ya shambulio hilo, vyombo vya usalama vimeongeza jitihada, huku kukiwa na mikakati kumkamata Kemunto.

Mwanahabari huyo aliyegeuka kuwa mfuasi wa kundi la kigaidi alikuwa mke wa Ali Salim Gichunge ambaye alitekeleza shambulio la kigaidi kwenye jumba la 14 Riverside Complex, (DusitD2), Januari 15, 2019.

Watu 21 akiwemo Gichunge waliuawa.

Washambuliaji wengine wanne walikuwa Omar Abdi Siyat, almaarufu Samatar, Hassan Abdiweli Gedi, almaarufu Osman Ibrahim Gedi na Mahir Khalid Riziki, na Mahir Riziki, mshambuliaji wa kujitoa mhanga.

Kemunto, anayejulikana pia kama Khadija Mahmoud, alikuwa Somalia wakati wa shambulio hilo. Ujasusi unaonyesha aliahidiwa maisha bora ikiwa angeunga mkono juhudi za jihad za mumewe.

"Alijua mipango na utekelezaji wa shambulio hilo kabla ya Gichunge na msimamizi wake huko Jilib, Somalia, kumhakikishia na kumuahidi mwisho mwema na kumshauri aikimbie nchi kupitia mpaka wa Mandera na Somalia kabla ya shambulio hilo," maelezo ya vyombo vya usalama yalisema.

Kabla ya kwenda Somalia, alikuwa mwanafunzi wa nyanjani katika Taasisi ya Ukuzaji Mitaala ya Kenya (KICD) mwaka wa 2014, katika idara ya uhusiano mwema nafasi ambayo alitumia kukusanya taarifa za kundi la kigaidi kabla ya shambulio la kigaidi.

Mume wake akiwa ameondoka na kukimbilia Somalia, Kemunto alisalia mikononi mwa wanamgambo wa al-Shabaab.

Taarifa ya kijasusi inasema aliolewa na kamanda wa ngazi ya kati kusini mwa Somalia ambaye baadaye aliuawa wakati wa makabiliano na Jeshi la Taifa la Somalia.

Baadaye aliolewa tena na mpiganaji wa al Shabaab, lakini mwanamume huyo aliuawa kwenye mpaka wa Kenya baada ya kuweka kilipuzi kwenye barabara ya Elwak-Mandera.

Kwa sasa Kemunto anaishi Jilib, eneo la makao makuu ya al Shabaab, ambako anafundisha lugha kwa watoto wa wanamgambo wa Al Shabaab.

Mwandishi huyo wa habari, baada ya kupata shahada yake ya uandishi wa habari na mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Masinde Muliro mwaka 2011, anajiunga na orodha ya wanawake waliodanganywa na kubadilishwa kwa itikadi kali na al Shaabab kwa ahadi za maisha mazuri.

Kemunto alikulia maisha yake ya utotoni jijini Nairobi. Alisomea Shule ya Msingi ya City mtaani Ngara, ambako alipata Cheti cha KCPE kwa alama 350, na baadaye akajiunga na Shule ya Upili ya Hamdan Girls iliyoko Mbale, Uganda.

IMETAFSIRIWA NA KUHARIRIWA NA DAVIS OJIAMBO.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved