logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Benny Hinn aomba msamaha kwa unabii wa uongo katika mikutano yake ya injili (video)

Mapema mwaka huu, Hinny alifanya mkutano mkubwa wa injili nchini Kenya uliohudhuriwa na rais.

image
na Radio Jambo

Burudani21 May 2024 - 01:31

Muhtasari


• “Baadhi yao walikwenda Zaidi ya ukombozi, na unajua kitu chochote Zaidi ya ukombozi sio unabii. Hatupaswi kuruhusu hilo kufanyika, mimi niliruhusu lakini nilikuja nikapiga marufuku."

amepangwa kufanya krusedi katika uwanja wa Nyayo

Mwinjilisti maarufu duniani mwenye asili ya Israel kutoka Marekani, Benny Hinn ameomba radhi kwa kuruhusu kile alichokitaja kuwa ni baadhi ya watu kutoa ushuhuda na unabii wa uongo katika mikutano yake ya injili.

Akizungumza kwenye podikasti moja, Hinn alijutia kuruhusu unabii wa uongo kutaradadi katika baadhi ya mikutano yake ya injili katika sehemu mbalimbali duniani, akisema kwamba anajuta kwa vitendo hivyo.

Mwinjilisti huyo maarufu kwa mahubiri yake runingani alisema kwamba yeye ni binadamu na wakati mwingine anateleza, hivyo kuwataka wanaofuatilia mahubiri yake runingani kutoka sehemu mbalimbali duniani kumsamehe.

“Sisi ni binadamu, na sisi wote hufanya makosa. Kama kuna vitu viwili ambavyo ninavijutia katika huduma zangu za injili ni kwamba sikuwa na busara ya kutosha kwa mara kadhaa na ushuhuda wa unabii. Nilikuwa na wageni ambao walikuja katika mikutano ya injili ambao nafikiri walizua balaa si tu kwa maisha ya watu lakini pia kwa taswira ya heshima yangu kwa sababu unabii wao haukuwa unabii wa kweli,” Hinny anaonekana akizungumza kwa majuto.

Mchungaji huyo ambaye mapema mwaka huu alikuwa na mkutano mkubwa wa injili nchini Kenya alikiri kwamba baadhi ya wageni wake katika mikutano ya injili walikuwa wanakwenda Zaidi ya shuhuda za ukombozi, akisema kuwa huo bila shaka ni uongo.

"Kuna wakati nilifikiri Mungu amenionyesha na nilizungumza. Cha kusikitisha ni kwamba natamani nirudi nyuma na kulikabili. Kuna baadhi ya unabii haukuwa sahihi au kutoka kwa Bwana. Kwa hilo naomba watu wanisamehe. Mimi ni binadamu tu.”

“Baadhi yao walikwenda Zaidi ya ukombozi, na unajua kitu chochote Zaidi ya ukombozi sio unabii. Hatupaswi kuruhusu hilo kufanyika, mimi niliruhusu lakini nilikuja nikapiga marufuku. Lakini hiyo ilikuwa ni miaka Fulani nyuma ambapo nilisimamisha,” aliongeza.

Itakumbukwa wakati wa hafla yake ya uponyaji nchini Kenya mapema mwaka huu ambayo ilihudhuriwa na rais William Ruto na mama wa taifa Rachel Ruto, moja ya tukio lililogonga vichwa vya habari ni binti wa kwanza wa taifa Charlene Ruto kujongea mbele na kutaka kuombewa kupata mume.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved