Mshambuliaji wa timu ya Al Hilal inayoshiriki Saudi Pro
League Neymar Jr, amerejea kucheza soka baada ya kupata jeraha la goti
lililomweka nje kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Neymah alirejea kusakata kabumbu katika mechi kati ya Al
Hilal na Al-Ain iliyokamilika kwa ushindi wa Al-Hilal wa mabao 5 kwa 4 kwenye
ligi ya klabu bingwa barani Asia.
Mchezaji huyo raia wa Brazil aliingia mchezoni akichukua nafasi
ya Nasser Al-Dawsari aliyepata jeraha katika dakika ya 77 ya mchezo.
Jeraha la Neymah limemweka nje kwa takribani siku 369.
Neymah alipata jeraha hilo akichezea timu ya taifa katika mechi ya kufuzu kombe
la dunia la mwaka 2026dhidi ya Uruguay mnamo October 17, mwaka wa 2023.
“Nahisi vizuri, ni ngumu lakini. Siku zote nina timu nzuri lakini nina
furaha sana nimerudi.” Alisema Neymah baada ya kucheza mechi
aliyoingizwa kipindi cha pili.
Wakati wa kupata jeraha, mchezaji huyo alikuwa amejiunga na
Al Hilal miezi 2 tu akitokea Paris Saint Germain kwa kitika cha Yuro milioni
90.