Waandalizi wa mbio za marathon za mjini Valencia
wametoa dau nono la hadi shilingi milioni 135 pesa za Kenya kwa mwanariadha
yeyote atayakevunja rekodi vya dunia inayoshikiliwa na hayati Kelvin Kiptum.
Mbio hizo zitafanyika Desemba 1 katika jiji la
Valencia nchini Uhispania kuanzia majira ya saa nne asubuhi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, waandalizi
wametangaza zawadi ya taslimu ya shilingi milioni 135 kwa mwanariadha yeyote
atakayevunja rekodi ya Kiptum ya 2:00:35.
"Tunataka kutangaza kwamba atakayevunja rekodi ya dunia atapata
euro milioni moja, ikiwa atavunja huko Valencia, bila shaka. Paco Borao atatoa
nusu moja nami nitampa nusu nyingine," alisema Juan Roig,
mwandalizi mwenza wa mbio hizo.
Wanariadha 3 kutoka Kenya wanatarajiwa kushiriki katika
kitengo cha wanaume katika mbio za marathon; Sabastian Sawe, Hillary Kipkoech
na Daniel Mateiko.
Sadfa ni kwamba Wote watatu wamepangwa kuanza marathon yao
ya kwanza.
Rekodi za sasa za ulimwengu katika kategoria za wanaume na
wanawake zinashikiliwa na Wakenya.
Ruth Chepngetich anashikilia rekodi ya wanawake baada ya
kuweka rekodi ya mwendo wa 2:09:56 katika mbio za 2024 za Chicago Marathon.
Rekodi ya wanaume inashikiliwa na marehemu Kelvin Kiptum.
Utendaji wa Kiptum katika mbio za Chicago Marathon za 2023
zilipamba vichwa vya habari duniani. Muda wake wa mbio za chini ya 2:01 wa
marathon sio tu kwamba aliweka rekodi mpya ya ulimwengu lakini pia alimweka
kijana mwenye umri wa miaka 24 kama mmoja wa vipaji vya kuahidi katika historia
ya marathon.
Hata hivyo, alikufa kwa kusikitisha katika ajali ya gari mnamo Februari na hivi karibuni aliadhimishwa na ukumbusho wa kuhakikisha urithi wake unaishi katika mitaa ya Chicago.