logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gor Mahia yacharaza Mara Sugar Homabay

Austin Odhiambo na Gideon Bandeka walitia kimyani mabao yaliyohakikishia Gor Mahia ushindi.

image
na Tony Mballa

Michezo30 November 2024 - 23:13

Muhtasari


  • Ushindi huo ulitamatisha msururu wa matokeo duni K’Ogalo walikuwa wameandikisha msimu huu kabla ya mechi hiyo.
  • Kocha Leonardo Neiva, raia wa Brazil, alijipata mashakani alipotimuliwa baada ya mashabiki kumwelekezea gadhabu kutokana na utendakazi usioridhisha.


           Wachezaji wa Gor Mahia washerehekea bao lao dhidi ya Mara Sugar



Gor Mahia walikwea hadi nafasi ya tano kwenye jedwali la Ligi Kuu ya Kenya baada ya kuandikisha ushindi wa 2-0 dhidi ya Mara Sugar katika uwanja wa Raila Odinga huko Homa Bay.

Austin Odhiambo na Gideon Bandeka walitia kimyani mabao yaliyohakikishia Gor Mahia ushindi.

Ushindi huo ulitamatisha msururu wa matokeo duni K’Ogalo walikuwa wameandikisha msimu huu kabla ya mechi hiyo.

Kocha Leonardo Neiva, raia wa Brazil, alijipata mashakani alipotimuliwa baada ya mashabiki kumwelekezea gadhabu kutokana na utendakazi usioridhisha.

Wasimamizi wa klabu waliteua mchezaji wa zamani Zedekiah ‘Zico’ Otieno kuchukua hatamu za uongozi huku wakiimarisha kampeni yard kutafuta kocha mpya.

Jumamosi, aliyekuwa Waziri Mkuu na mlezi wa Gor Mahia Raila Odinga alikuwa miongoni mwa mashabiki walioshuhudia ushindi huo muhimu wa K'Ogalo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved