
KARIM Benzema hakubaliani na Cristiano Ronaldo kwamba yeye ndiye mchezaji bora wa wakati wote - badala yake, anaamini Ronaldo Nazario anashikilia sifa hiyo.
Gwiji huyo wa Real Madrid alicheza na mshindi huyo wa tuzo ya
Ballon d'Or mara tano kwa miaka tisa nchini Hispania, akijiunga na klabu hiyo
pamoja naye na nguli wa AC Milan, Kaka mwaka 2009.
Licha ya kushuhudia rekodi nyingi alizoweka mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 40 katika kipindi chake cha kusisimua kwenye La Liga,
haikutosha kumfanya kuwa mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea, machoni pa
Benzema.
Benzema, ambaye aliondoka Uhispania na kujiunga na klabu ya
Al-Ittihad ya Saudi Pro League mnamo 2023, pia alimpuuza nyota wa Barcelona
Lionel Messi alipoulizwa kuhusu maoni ya hivi majuzi ya Ronaldo kwamba anaamini
kuwa yeye ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kupamba uwanja wa soka.
"Kila mtu anaweza kusema anachotaka. Ikiwa anadhani yeye ndiye
bora zaidi katika historia, sawa, basi ni yeye," mchezaji huyo wa
miaka 37 alisema.
"Kwangu mimi, kwa mfano, ni Ronaldo, yule kutoka Brazil. Lakini
Cristiano ndivyo alivyo. Sipendi kulinganisha wachezaji; naamini kila mmoja ana
hadithi yake, na ana yake, ni mzuri sana."
Nyota huyo wa Al-Nassr alizua hasira kwa kauli yake ya
kujiamini, akitaja maisha yake marefu katika kiwango cha juu na idadi ya mabao
kuwa sababu zinazomfanya aamini kuwa yeye ndiye mkubwa zaidi.
"Kwa kweli
sijaona mtu yeyote bora kuliko mimi. Lazima uangalie nambari kamili,"
alisema katika mahojiano na kituo cha Uhispania El Chiringuito.
"Ninaamini mimi ndiye mchezaji kamili zaidi aliyewahi kuwepo. Ni
mimi. Nafanya kila kitu kwenye soka. Nacheza vizuri katika suala la kupiga
mpira wa kichwa, nina uwezo wa kupiga mipira ya adhabu, niko vizuri kwa mguu
wangu wa kushoto, nina haraka, nina nguvu, ninaruka. Mimi ni mchezaji bora
kuwahi kutokea, naamini hivyo."
Mchezaji mmoja ambaye alichukizwa na tamko la Ronaldo ni
mchezaji mwenzake wa zamani, Angel Di Maria. Muargentina huyo ni mmoja wa
wachache waliocheza na fowadi wa Ureno na Messi na ana maoni tofauti.
"Yeye [Ronaldo] kila mara alitoa matamshi ya aina
hii," Di Maria alikiambia chombo cha habari cha Argentina Infobae.
"Siku zote alijaribu kuwa bora, lakini kwa bahati mbaya alizaliwa katika
kizazi ambacho kulikuwa na mchezaji mwingine [Messi] ambaye alifanya kila
alichogusa kugeuka kuwa dhahabu.
"Ukweli unaonyeshwa katika nambari. Mchezaji mmoja
alishinda tuzo nane za Ballon d'Or [Messi] huku mwingine akishinda tano
[Ronaldo]. Tofauti nyingine muhimu ni kwamba mmoja ameinua Kombe la Dunia
[Messi]. Kuna tofauti nyingi kati ya wachezaji hao wawili."