
MARSEILLE wametishia kujiondoa Ligue 1 na kujiunga na Ligi ya European Super League kufuatia kushindwa kwao na Auxerre siku ya Jumamosi, huku rais wa klabu hiyo Pablo Longoria akidai kuwa ligi hiyo "imechakachuliwa".
Maresille ilichapwa 3-0 na Auxerre, huku mabao mawili kati ya hayo yakifungwa baada ya beki Derek Cornelius kutolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jeremy Stinat.
Matokeo hayo yanawaacha Marseille wakiwa nyuma ya vinara wa
ligi hiyo Paris Saint-Germain kwa pointi 13 baada ya kushinda mchezo wao
mkononi dhidi ya Lyon Jumapili.
Hata hivyo, Marseille walikasirishwa na kadi nyekundu ya
Cornelius, huku meneja Roberto De Zerbi akiapa kutofanya kazi tena Ufaransa
kutokana na mwamuzi huyo wa "kashfa".
"Mimi ni Muitaliano,
na baada ya OM sitaenda kufundisha tena Ufaransa," alisema.
"Kuna tatizo katika michuano ya Ufaransa, ikiwa
Wafaransa wanafurahishwa na kiwango hiki cha maamuzi, basi ni nzuri kwao. Lakini
leo ilikuwa ni kashfa. Mwamuzi hakuwa katika [hali sahihi ya akili kuchezesha]
mechi hii kwa sababu ya mabishano yote yanayomzunguka."
Mapema mwaka huu, mkurugenzi wa kandanda wa Marseille Mehdi
Benatia alifungiwa kwa miezi mitatu kutokana na tabia yake katika mechi ya
Coupe de France ya Marseille dhidi ya Lille.
Benatia alitolewa nje kwa kadi nyekundu na Clement Turpin
baada ya kumkosoa afisa wa nne Stinat baada ya Marseille kutopewa penalti.
Marzeille walikuwa wameelezea wasiwasi wao kuhusu uteuzi wa
Stinat kwa pambano lao na Auxerre.
Baada ya mchezo huo, rais wa klabu Longoria alinukuliwa
akisema na La Provence: "Kila kitu kimepangwa. Kimepangwa,
kimechakachuliwa.
"Kuna penalti juu ya
Merlin, waamuzi wanne wa Ulaya wameniambia hivyo kwa ujumbe, na jambo la kashfa
zaidi ni kadi nyekundu kwa Cornelius. Huu ni ubingwa wa sh***y, ikiwa Super
League itakuja kutuona, tutaenda mara moja."