
UCHUNGUZI wa polisi umeanzishwa nchini Ecuador baada ya mke na mtoto wa beki wa C.S. Emelec Jackson Rodriguez kutekwa nyara.
Kulingana na jarida la The Mirror, tukio hilo lilitokea
asubuhi ya Jumatano mwendo wa saa 2.50 asubuhi katika jiji la Guayaquil.
Beki huyo wa pembeni mwenye umri wa miaka 26 inasemekana
aliambia mamlaka kwamba alijificha chini ya kitanda chake aliporipotiwa kusikia
mlango wake wa mbele ukivunjwa na gobore kubwa.
Mchezaji kandanda huyo pia amewaambia polisi kwamba baada ya
kuchungulia nje ya dirisha aligundua watu hao "walikuwa wakisafiri kwa
lori la rangi ya kijivu."
Kulingana na ripoti za polisi, washukiwa hao walikuwa
wameuliza aliko Rodriguez baada ya kuingia kwenye mali hiyo kabla ya kuwateka
nyara mke wa mchezaji huyo na mtoto wake mdogo.
Guayaquil, mji mkuu wa jimbo la Guayas na ambapo tukio hilo
lilitokea, umekuwa chini ya tamko la "mgogoro wa ndani wa silaha"
tangu Januari 2024.
Si mara ya kwanza ambapo Mucho Lote 2, mtaa unaojadiliwa,
kumekuwa na tukio la utekaji nyara.
Mnamo Januari 6 utekaji nyara mkali uliacha jamii ya eneo
hilo ikishangazwa na tangu wakati huo kumekuwa na video za majaribio ya utekaji
nyara ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Wakati wa kisa hicho mnamo Januari, mmiliki wa duka
alichukuliwa na watu wenye silaha, ambao pia walivunja mlango wake, kabla ya
kumpiga.
Vyanzo vya ndani vinadai mwathiriwa alidaiwa kulipa dola
10,000 ili kuachiliwa, ingawa washambuliaji walikuwa wakidai awali $ 50,000.
Rodriguez amewaambia polisi kuwa hajapokea ujumbe wowote wa
vitisho kabla ya tukio hilo.
Mnamo Desemba, mwanasoka mwenzake Pedro Perlaza alitekwa
nyara alipokuwa akiichezea Liga de Quito na akaokolewa na mamlaka siku chache
baadaye.
Beki Rodriguez, 26, amecheza mechi tisa za LigaPro Serie A
msimu huu kwa Emelec, ambao bado hawajazungumza chochote kuhusu matukio
yaliyotokea. Mnamo 2023, winga wa Liverpool Luis Diaz aliunganishwa tena na
baba yake Luis Manuel Diaz siku 12 baada ya kutekwa nyara na Jeshi la Ukombozi
la Kitaifa (ELN) huko Colombia.