Wapo wengi waliokuwa wanajiuliza maswali mengi yasio na majibu kuhusu ukimya wake msanii aliyeimba ngoma hatari ya Muziki, Darassa.
Baada ya kupotea kwa muda mkali huyu amerudi tena kwenye gemu na kutikisa anga za burudani na kibao kinachofahamika kama Leo akimshirikisha msanii Jux.
Nguli huyu anafahamu kwamba alikuwa amepotea katika muziki kwa kipindi kirefu zaidi na huenda ukimya wake uliwashangaza mashabiki, wanaopenda muziki wake wa mashairi na kwa hivyo anaanza kwa kuomba msamaha kwa kuchelewesha ngoma katika video hiyo ya dakika tatu.
“Hello it’s me again Mr Burudani take away the pain kwa kuchelewa si unajua foleni nawapa vidonge kutuliza complain”, anasema darassa katika laini ya kwanza ya kichupa hichi cha Leo.
Ngoma hii imerekodiwa na kuongozwa na Hascana katika mandhari mazuri zaidi na ya kuvutia. Ngoma hii inafanya vizuri katika mtandao wa Youtube na kuchezwa katika vyombo kuu vya utangazaji hapa Afrika Mashariki.
Mkali huyu wa mashairi kushirikiana na Jux katika ujio wake mpya ni jambo ambalo mashabiki wengi hawakukusudia. Beat ya ngoma hii ni ya kilabu kabisa na ya kuchezesha.
Mwanzoni mpaka mwisho video yake imerembeshwa na vichupa vyenye haiba ya juu zaidi.
Kando na muziki huu alioufanya na Jux, ameweza kuingia studio na mwanadada aliyetisha na kibao “Niokote” kinachokwenda kwa jina Tumepoteza.
Inaashiria kwamba mkali huyu amerudi katika anga za burudani ili kuzidisha kuwakonga nafsi mashabiki wake.