Sheilla Akwara ni mojawapo ya watoto waliopitia katika mazingira haya ya maonevu.
Mwanadada huyu aliihama nchi yake na kuzamia Marekani ili kupata masomo zaidi.
https://www.instagram.com/p/B5SP-2ogXJ1/
Akisimulia Bustani la Massawe maisha yake, Sheila amesema kuwa alichukizwa na jinsi shuleni alikuwa anapata kichapo cha mbwa.
"Shuleni tulipigwa na walimu kinyama. Shule hiyo nilihamia baada ya kutofanya vizuri katika shule niliyosomea..." Sheila akisimulia Massawe.
https://www.instagram.com/p/B5ShG0bAMu8/
Kuchapwa kila mara kulimuumiza kisaikolojia na kuona thamani yake haipo na hivyo akaamua kujitoa uhai.
Hakuweza kuangamia kwani alipata usaidizi wa dharura na kukwepa mauti.
Kwa sasa Sheila anafanya juhudi za kuhamasisha jamii kuhusu kuwapiga na kuwadhalimu watoto wadogo.
Sheila anawahamasisha watu kuhusu maisha na kutoa msisitizo kwa wazazi kuwasikiliza wanao kwa kiwango kikubwa badala ya kuwaadhibu.
Mwanadada huyu hakupenda mazingira ya pale nyumbani kwao,
"Uncle walikuwa wakija kwetu na kusema kuwa mama amezaa wasichana ambao hawawezi kumsaidia. Walitaka awe na wavulana." Alisema Sheila.
Aidha presha za wazazi awe mhandisi au daktari zilimnyima uhuru wa kuchagua anachotaka maishani.
"Wazazi wanataka ukue mhandisi au daktari..." Sheila alizidi kusema.
Kuhusu nia na azma ya kutoka Marekani, mwanadada huyu amesema kuwa hakufurahishwa na vitendo ya wanarika kujiua.
"Nilikuona nikiona story hizi kwa social media watu walijiua kwa sababu ya depression. Nilirudi kuhamasisha watu. Kwa nini watu wajiue? Ni presha nyingi ya wazazi na jamii..." Alisema Sheila.
"Naambia watu wakuwe na vision. Nilipoenda Marekani maisha yalikuwa rahisi,nilidhani nitaishi na depression maisha yangu..." Sheila.