logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wakwezangu wamlisha kuku mweusi nywele na kucha zangu

Wakwezangu wamlisha kuku mweusi nywele na kucha zangu

image
na

Football02 October 2020 - 05:31
Ni vituko vya maajabu ambayo watu hupitia endapo watachukua hatua ya kwenda kwa mganga ili watibiwe na kutatuliwa shida zao za kifamilia.

Lakini kwa mwanamke Evelyne ni tofauti sana kwa maana alijipata kwa mganga baada ya kupelekwa na wakwe zake.

"Nilibeba mimba nikiwa kidato cha pili, ilinilazimu nitoke shuleni, lakini uja uzito wangu ulitoka mapema, huku ikinilazimu niende kushi na shangazi yangu

Lakini baada ya miezi 11, aliaga dunia na maisha yangu yakabadilika mara moja." Alieleza Evelyne.

Baada ya maisha yake kubadilika Evelyne alipata kipenzi cha roho yake na kuamua kufunga ndoa, hapo ndipo alijua ya Mola ni mengi lakini ya kuku ni mayai.

" Wakwezangu walinipigia simu na kuniambia kuwa mama mkwe wangu amefariki kwa hivyo napaswa kuenda nyumbani,

Keshoye mume wangu alipoenda kazini, wakwe wangu waliniambia niingie kwa kijumba cha mabati, tulikaa hapo nikiwa na dada zangu, mama mkwe na mganga

Pia kulikuwa na besheni iliokuwa na maji yenye rangi ya kijani kibichi, kuku mweusi, kitita cha pesa na  shuka jeupe la kutandika kitanda." Alisimulia.

Evelyne hakunyamaza aliwauliza kwanini walimpeleka kwa mganga walikuwa na haya ya kusema,

"Kwa maana mama mtu alipiga simu na kusema mama yetu ameaga ilhali hakuwa ameaga, na kwa maana ni mlevi ndio maana tumekuleta hapa tumsaidie aache ulevi

Na kama mwana wake unapaswa kumsaidia." Alizungumza.

Alishtuka tu wakati mganga alianza kufanya sarakasi zake za kumkata nywele na kucha.

" Mganga alinikata nywele na kucha, baada ya kufanya hivyo alimwambia kuku huyo apanue mdomo na akala nyele na kucha zangu

Kwa maana nilikuwa na uja uzito, kesho yake nilienda kujifungua, na kubarikiwa na mapacha, wa kwanza alikuwa kijana ambapo nilipojifungua 

Maji ya manjano yalianza kutoka iliwabidi madaktari wanitoroke, walirudi na kutoa mtoto wa pili ambaye alikuwa wa kike

Baada ya kujifungua watoto wangu walipelekwa kwa chumba cha watoto, baada ya muda mtoto wa kwanza alianza kutetemeka nami pia nikaanza kutetemeka 

Daktari alikuja kuniharifu kuhusu ya kisa hicho lakini alinipata pia nami na tetemeka, mtoto wangu aliaga, kesho kibaridi hicho kilikuja kinikitengenezea mtoto maziwa

Mtoto wangu alianza kutetemeka nami pia nikaanza kutetemeka mtoto wa pili akaaga dunia." Aliongea.

Uchawi huo ulimfanya Evelyne kupoteza watoto wake wawili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved