logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ishara zinazoonyesha mwanamke anakupenda kwa ajili ya pesa zako

Ikiwa unajiuliza ikiwa mpenzi wako amekupenda kwa ajili ya pesa zako

image
na Radio Jambo

Michezo15 June 2021 - 10:31

Muhtasari


  • Huku Wakati wanawake wengi wana wasiwasi mwanamume anamtumia au kumpenda kwa ajili ya ngono
  • Ishara zinazoonyesha mwanamke  anakupenda kwa ajili ya pesa zako

Huku Wakati wanawake wengi wana wasiwasi mwanamume anamtumia au kumpenda kwa ajili ya ngono, wanaume wengi, haswa katika nyakati hizi ngumu za kiuchumi wana wasiwasi kuwa wanawake wanawapenda kwa ajili ya pesa zao.

Ikiwa unajiuliza ikiwa mpenzi wako amekupenda kwa ajili ya pesa zako, husitie shaka kwani nitakupa ishara zinzoonyesha anataka tu pesa zako.

1.Halipi Gharama

Kama umejuana na mwanamke wako kwa muda, endapo mumeenda kujivinjari anapaswa kujitolea na kulipia gharama na baadhi ya vitu na wala sio kuketi na kungoj tu ulipe kila kitu.

2.Unapoishiwa na pesa 

Kuishiwa na pesa aje yaani ukianza kuwa broke, haya basi jua umenyonywa pesa bila ya huruma, na mwanamke huyo hajali kile unapitia.

3.KUwa na shida na pesa kila wakati'

Kama mwanamke kamili unapaswa kujisimamia baadhi ya gharama zingine na wala sio kumtegemea mwanamume wako pia naye anamahitaji yake ya kutimiza

Kila mara mnapokutana anataka tu pesa.

4. Uhusiano wako ni wa kiwango cha juu

Anaepuka mazungumzo ya uhusiano kama pigo na mara nyingi anasema 'wacha tuone ni wapi mambo yataenda' lakini hajitolei kwako.

 Hujui chochote juu ya marafiki na familia yake na yeye hajui chochote juu ya maisha yako, hata jina lako la mwisho

5.Vitu vinavyoenda mrama unapokuwa 'broke'

Ikiwa anakuuliza umtumie pesa ya mavazi lakini unasema kuwa huwezi, utagundua kwa mtazamo wake jinsi atakuepuka na endapo utamtumia pesa haya basi anarudisha tabasamu yake, na kukupa mahabara kweli kweli.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved