logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mombasa: Wachuuzi wa ngono warejelea kutoa huduma hizo kwa wanabodaboda

Wamerejelea kutoa huduma za ngono kwa kuhofia kupoteza wateja wao ambao ni wanabodaboda.

image
na Radio Jambo

Habari18 March 2022 - 05:35

Muhtasari


• Walisema wameafiia kurejelea biashara hiyo kwa kuogopa kuwapoteza wateja baada ya kusitishwa kwa wiki moja.

Makahaba (Picha; Maktaba)

Ni afueni kubwa kwa wanabodaboda mjini Mombasa baada ya wadangaji kusitisha marufuku yao waliyoiweka dhidi ya kuwauzia ngono wanabodaboda wiki iliyopita.

Marufuku hiyo iliyodumu kwa muda wa wiki moja sasa imefutiliwa mbali na wadangaji hao na kusema sasa wako tayari kufanya biashara ya miili yao na wanabodaboda hao baada ya kupewa msamaha na serikali.

Ikumbukwe wiki jana wanabodaboda walijipata pabaya kote nchini kutokana na kusambaa kwa video iliyowaonesha wakimdhulumu na kumpiga mwanamke mmoja aliyetajwa kuwa mwanadiplomasia kutoka Zimbabwe.

Serikali ilitangaza bodaboda zote kuondolewa barabarani mpaka mipango Madhubuti itakapowekwa ili kuilainisha sekta hiyo ambayo imejawa na mahuni wanaojifanya wanabodaboda.

Hapo ndipo pia vuguvugu la wadangaji jijiniMombasa walitangaza kusitisha kuwapa huduma wanabodaboda kwa kumdhulumu mwanamke katika barabara ya Forest jijini Nairobi.

Kupitia kwa mkurugenzi wa vuguvugu linalotetea haki za wadangaji nchini, watoa huduma za ngono wameamua kusitisha marufuku yao kwa kuhofia kuwapoteza wateja wao.

Uvumi unasema kwamba jiji la Mombasa linadaiwa kuwa na wadangaji zaidi ya elfu kumi waliojiandikisha katika vuguvugu hilo.

Haya basi wanabodaboda msinyongonyee huduma zimerudi!


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved